Na Swaum Katambo,Site Tv Nsimbo-Katavi Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umeanza utekelezaji wa wa kipindi cha Pili cha awamu ya tatu ya TASAF ambapo ruzuku kwa walengwa zitafanyika kwa njia ya Mtandao nchi nzima. Akitoa Hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wakuu wa Idara na mafunzo ya wawezeshaji wa Halmashauri kuhusu Utekelezaji wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF na uhakiki wa Kaya za walengwa wa Mpango wa kunususru Kaya Masikini uliofanyika katika Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi Josephine Pupia alisema kipindi hiki cha pili kitatekelezwa katika Halmashauri zote 185 za Tanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar. "Utekelezaji huo utafanyika kwenye Vijiji/Mitaa/Sehia zote nchini na kujumuisha maeneo ya Vijiji/Mitaa/Sehia ambayo hayakupata Fursa hiyo katika kipindi cha kwanza cha utekelezaji wake ambacho kimekamilika." Alisema Bi.Rupia Kulia (aliyevaa nguo ya ...
Karibu kwenye Blog Yetu na tupo tayari kukuhabarisha kwa Habari na Matukio mbalimbali kwa Weledi Masaa 24 popote ulipo,kama una taarifa au unataka kutangaza na Sisi tafadhali wasiliana nasi kupitia ukurasa huu. Pia tunapatikana YouTube @sitetvtz,Instagram,Twitter na Facebook @sitetvtz. Ofisi zetu zipo Jengo la Mpanda Plaza Ghorofa ya 3,Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.