Nteghenjwa Hosseah, OR- TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo amewataka wateule wa Rais kuwa na mahusiano mazuri kazini na kusisitiza kuwa Rais John Magufuli anahuzunishwa na wateule wake kugombana badala ya kufanya kazi.
Jafo ametoa rahi hiyo kwa wateule 22 wa Rais, wakiwamo wakuu wa mikoa wawili, katibu tawala wa mkoa mmoja, wakuu wa wilaya 10 na wakurugenzi wa halmashauri nane ambao wameteuliwa na kuapishwa juzi Ikulu ya Chamwino Dodoma wakati wa kuwakabidhi nyenzo za kufanyia kazi.
Alisema suala la kuimarisha mahusiano kazini kati ya wateule na watumishi walio chini yao na kuwa Rais hafurahishwi na namna wanavyogombana badala ya kufanya kazi.
“Haipendezi kukuta, mkuu wa mkoa anagombana na mkuu wa wilaya, au mkurugenzi na mkuu wa wilaya kazi haziendi kwasababu ya ugomvi wenu, kusema ukweli sitarajii viongozi nyinyi ambao Rais amewateua ili msaidie majukumu kuwaita kwenye vikao kwa mambo ambayo ninyi wenyewe mnaweza kumaliza. “
Jueni kuwa mmechaguliwa si kwa upendeleo bali kwa uwezo wenu wa kufanya kazi na mmepewa kipande cha kumsaidia Rais kuwatumikia wananchi hivyo mkafanye kazi, kumbukeni kuwa mheshimiwa Rais (John Magufuli) hafurahishi na hali ya migogoro baina ya wateule wake au na watumishi.”
Jafo alisema ili kuondokana na migongano baina yao wanayopaswa kufanya ni kuzingatia na kuheshimu mipaka yao ya kazi. “
Kila mtu akafanye kazi katika mipaka yake ya kazi, sio muende huko mkuu wa mkoa anawaza kumfunika mkuu wa wilaya, au mkuu wa wilaya anataka kumfunika mkuu wa mkoa, na matatizo haya yako sana kwenye maeneo ya mijini na ndio maana unaona hata kufungua choo kimoja anataka kwenda Mkuu wa mkoa, mkaheshimu na kuzingatia mipaka yenu ya kazi.”-Alisema Waziri Jafo
Aidha, Jafo amewataka viongozi hao kuwa na nidhamu na kuhakikisha watumishi walio chini yao wanafanyia kazi kwa nidhamu katika nyanja zote na kusisitiza kuwa ufanyaji kazi kwa mazoea halikubaliki.
Pia amewataka kuzingatia maadili ya viongozi wa umma katika nyanja zote na kuwahimiza wanapofika kwenye maeneo yao ya kazi wasiende kutengeneza maadui bali marafiki ambao watafanya kazi kwa ushirikiano.
Mhe. Jafo pia amesisitiza viongozi hao kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika vita ya kupambana na dawa za kulevya katika maeneo yao
“Serikali haitaki kuona wananchi wake badalaya ya kufanya kazi wanajikita katika matumizi ya dawa za kulevya, ushiriki wa wananchi katika kufanya kazi pia kumechangia Tanzania kufika kwenye uchumi wa kati hata kabla ya muda tuliojiowekea, hivyo vita ya dawa za kulevya ni ya viongozi katika ngazi zote, hakikisheni mnalisimamia hilo.”-Alisema Mh. Jafo
Jafo pia alisema viongozi hao wanapaswa kuhakikisha hoja za ukaguzi za CAG zinajibiwa kwa wakati na kusisitiza kuwa hataki kusikia halmashauri inakuwa na hati chafu hasa ikizingatia kuwa kazi kubwa imefanyika mpaka kufanya taarifa ya cag ya hivi karibuni inaonesha kuwa asilimia 95 Ni hati safi na asilimia 5 zinamashaka.
Jafo wamewasisitizs viongozi hao katika kuhakikisha wanasimamia mkusanyo ya mapato na matumizi ya fedha za ndani.
Pia amewataka kuhakikisha asilimia 10 zinazopelekwa kwa vijana, wanawake na wenye ulemvu zinawafikia walengwabna kuwa kinyume chake ni kukiuka Sheria kwasababu suala liko kisheria.
(Mwisho)
Comments
Post a Comment