Na Swaumu Katambo, Katavi
Wafanyabiashara wadogo katika stendi ya mabasi Mizengo Pinda wameiomba Serikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuepukana na adha ya kulipa ushuru wa Halmashauri ambao una gharama kubwa.
Wakizungumza na Site Tv wajasiriamali Mjini Mpanda wameilalamikia Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kucheleweshwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki.
Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote.
MWISHO
Comments
Post a Comment