Skip to main content

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe Jamila Yusuph akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe Jamila Yusuph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021.

Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021.
Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe Jamila Yusuph akiondoka katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga mara baada ya kumalizika Misa ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021.

Na Mathias Canal, Mlele-Katavi

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe Jamila Yusuph amesema Wilaya ya Mlele itamkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli kwa Maendeleo aliyoyafanya.

Mhe Jamila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye Misa maalumu ya kumuombea Dkt Magufuli iliyofanyika leo tarehe 24 Machi 2021 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi.

Dc Jamila amesema kuwa miongoni mwa mambo mahususi ambayo wananchi watamkumbuka kwa kina Hayati Dkt Magufuli ni pamoja na Uimarishwaji wa huduma za Afya, Miundombinu ya Barabara, Mawasiliano na Uchukuzi, Uboreshwaji wa Huduma za Maji, Sekta ya Elimu ikiwa ni pamoja na Miradi ya Umeme mijini na vijijini.

Kadhalika DC Jamila ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kupokea kijiti katika kipindi cha majonzi huku akiamini kuwavusha watanzania kufikia katika dhamira ya Tanzania waitakayo.

Akizungumza wakati wa Ibada hiyo Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri Maricelo Butoyi amesema ili kumuenzi Hayati Dkt John Pombe Magufuli ni lazima kuyaenzi matendo yake kwa kuwa wazalendo hususani kukemea vitendo viovu ikiwemo Rushwa na ubadhilifu wa mali za umma.

Padri Butoyi, amewaomba wananchi kutumia muda wao kufanya ibada ya kuwaombea Viongozi wa Serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe Rachel Kasanda anayeendelea na matibabu pamoja na Taifa kwa ujumla wake.

Akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo MhSoud Mbogo amewaomba wananchi kumtanguliza Mungu na kufanya matendo mema aliyokuwa akiyafanya Hayati Rais Magufuli.

Kadhalika, amelipongeza Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga kwa kuendesha misa maalumu ya kumuombea Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli.

MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja