Skip to main content

MBIFACU KUKARABATI HOTELI WILAYANI MBINGA KUFIKIA VIWANGO VYA KIMATAIFA.

Muonekano wa hoteli ya MBICU utakapokamilika ukarabati wake ambao unafanyika kwa miaka mitatu.

CHAMA Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Mbinga Nyasa (MBIFACU) Mkoani Ruvuma kimeanza  mradi wa ukarabati wa  hoteli ya MBICU ambayo inamilikiwa na chama hicho ili iweze kuwa na  viwango vya kimataifa.

Alisema ukarabati wa hoteli hiyo ambao umeanza mwaka wa fedha wa 2019/2020 unatarajia kukamilika baada ya miaka mitatu na kwamba katika kutekeleza mradi huo zaidi ya shilingi bilioni moja zitatumika.

Hata hivyo alisema ukarabati wa hoteli hiyo unafanyika kwa awamu ambapo katika awamu ya kwanza yanajengwa majengo sita na kujenga uzio ambao utazunguka eneo lote la hoteli hiyo.

“Eneo hili litakuwa majengo 15 pamoja na jengo la hoteli,majengo yote yataezuliwa na kuezekwa katika mtindo wa kisasa  ili kukidhi viwango vya kimataifa na kuvutia wageni wa ndani na nje ya nchi’’,alisisitiza  Ndimbo.
Kaimu Meneja wa MBIFACU Henerick Ndimbo akitoa maelezo ya ukarabati wa hoteli ya MBICU
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa MBIFACU Winfred Lupembe alisema mara baada ya kukamilisha mradi huo wanatarajia kuongeza mapato makubwa kupitia hoteli ya MBICU ambayo wageni watakuwa wanapata malazi, chakula na hudumu nyingine.

Alisema kutokana na hoteli hiyo kuwa na hadhi ya kimataifa wanatarajia kupokea wageni wa kimkoa,kitaifa na kimataifa na kwamba  Bodi ya chama hicho imefanikiwa  kusimamia shughuli za ukarabati wa hoteli hiyo ambazo zinaendelea vizuri na wanatarajia kukamilisha kwa wakati.
Ukarabati wa vyumba vya kulala katika hoteli ya MBICU iliyopo mjini Mbinga
Bumi Masuba ni Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoani Ruvuma anasema kuwa hoteli ya MBICU ilijengwa miaka ya 1990 na kwamba ilisimama kutoa huduma kutokana na ubovu wa miundombinu yake.

Hata hivyo alisema MBIFACU wameamua kuifanyia ukarabati mkubwa hoteli hiyo  na mara baada ya ukarabati kukamilika hoteli ya MBICU itakuwa ni miongoni mwa hoteli bora zaidi katika Mkoa wa Ruvuma.

“Hoteli hii itakuwa ni ya kipekee katika Mkoa wa Ruvuma kwa sababu mgeni atapata mahali pa kulala,kula,kunywa,bustani maarufu ya kupumzikia,eneo la kuegesha magari,hii ni hoteli yenye eneo kubwa sana ina kila kitu,hapa itakuwa ni zero grazing’’,alisisitiza Masuba.
Majengo ya hoteli ya MBICU yanavyoonekana hivi sasa kabla ya ukarabati kufanyika
MBIFACU ni Chama cha Ushirika ambacho kilianzishwa Agosti 14,2020 na kinafanya shughuli zake katika wilaya za Mbinga na Nyasa,chama hicho pia kinatoa huduma kwa wakulima wanaolima kahawa wilaya ya Songea.

Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Julai 5,2020
Mbinga

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja