Na Aidan Felson,Site Tv
Mpanda,Katavi.
Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza,inatarajia kuwaunganishia Wateja wa Umeme wapatao 10,665 katika Vijiji 113 vya Wilaya zote Tatu za Mkoa wa Katavi.
Akisoma taarifa kwa Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Khamis Mgalu (MB),Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Rachel Kasanda alisema,Mradi huo kabambe wa Umeme unaotekelezwa na Kampuni ya CHINA RAILWAY CONSTRUCTION ELECTRIFICATION BUREAU GROUP (CRCEBG) ulianza Mwezi Februali,2019 kwa Gharama ya Tsh. Bilioni 43.1 na umefikia Asilimia 58.35.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Rachel Kasanda (Mkuu wa Wilaya ya Mlele).
"Na mpaka sasa hivi kazi inaendelea na ipo Asilimia 58.35,Jumla ya Mawanda wa mradi njia ndogo wenye Kilomita 551.2 na Jumla ya Mawanda Scop ya njia kubwa ni Kilomita 586.34 kulingana na Mawanda ya mradi wa REA awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza ulivyoainisha"-Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Rachel Kasanda.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Khamis Mgalu (MB) baada ya kupokea taarifa hiyo alionyesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa mradi huo kwani kati ya Vijiji 113 ni Vijiji 44 pekee ambavyo vimewashwa Umeme.
"Natambua kwamba mradi huu ulichelewa kuanza kwa Mkoa wa Katavi na Kigoma kutokana na changamoto za taratibu za manunuzi kupitia Mkandarasi wa kwanza ambaye alipata tenda ile lakini tukafanya tena kwa maslahi ya umma,hata Mkandarasi tangu mwezi wa pili 2019 ana miezi takribani 15 sasa tangu ameanza hii kazi,Kwahio kuwa chini ya asilimia 39 kama kuna mwakilishi wake nadhani baadae tutakutana kwakweli hii spidi bado"-Alisema Mh Subira Mgalu,Naibu Waziri wa Nishati.
Aidha,ameshitushwa na ghalama za uendeshaji wa uzalishaji Umeme kutoka Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Katavi ambapo kiasi cha Tsh. Milioni 21 kinatumika kwa Siku sawa na Bilioni 7 kwa Mwaka,na amesema kutokana na hali hiyo Serikali kupitia Shirika la TANESCO imeamua ije na mpango wa kati wa ujenzi wa Msongo wa Kilovoti 132 kutoka Sikonge Mkoani Tabora hadi Mpanda.
"Yapo maombi ya wadau,wanataka Umeme Level ya Megawati 1.1,ambazo hatuna,sababu ziada iliyobaki ni yakulinda Mashine,ya Kilowati 170,siyo ya kusema labda unaweza kumgawia Mwekezaji Mkubwa,kwahiyo ni wazi pia kwa ghalama hizi zinazoendelea Milioni 21 kwa siku,Milioni 648 kwa Mwezi,Bilioni 7 kwa Mwaka,za kuzalisha Umeme kwa Mkoa wa Katavi ni kubwa sana...Hali inavyoonekana hivi karibuni tutafikia matumizi ya juu kabisa,itoshe tu kusema hii ni kiashiria cha hatari,lazima tupambane mradi huu uendelee kwa kasi"-Mh. Subira Mgalu,Naibu Waziri wa Nishati.
Wajumbe wakiwa wanasikiliza taarifa na Maelekezo ya Naibu Waziri wa Nishati Ofini kwa Mkuu wa Mkoa.
Akiwa katika Kituo cha Afya cha Katumba Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda kuzindua na kuwasha Umeme katika Kituo hicho,Mh. Mgalu alimuagiza Mkandarasi ahakikishe anafikisha Umeme katika Kaya zaidi ya 100 na Nyumba za Watumishi wa Afya wanao hudumia katika kituo hicho,wawe wameunganishiwa Umeme hadi kufikia Tarehe 12 Mwezi huu.
Naibu Waziri wa Nishati (Aliyevaa Mtandio Kichwani) akikata utepe kuzindua Umeme katika Kituo cha Afya cha Katumba.
"Miradi hii,tija yake ni Wananchi kuunganishwa kwa mujibu wa wigo uliopo,Wateja wa awali,sasa wale wanaohitaji ambao wapo kwenye wateja wa awali wanalalamika,wale ambao wametajwa kwamba tutaanzia na nyinyi kutokana na Bajeti iliyopo hawaunganishwi kwa wakati,Umeme toka Mwezi wa Tatu,mazungumzo gani hayo na UN yasiyokamilika!?"-Mh. Subira Mgalu,Naibu Waziri wa Nishati.
"Mkandarasi kesho uanze kazi,Ole wako usipoanza. Mh,(Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Rachel Kasanda) utaniambia,na bado una kaimu na mwenyewe Mkuu (DC Mpya Bi. Jamila Yusuf) mkabidhi,ndo kazi yake ya Kwanza aisimamie hii hawa Watumishi wapate Umeme"-Naibu Waziri wa Nishati akiwa Ziarani Mkoani Katavi Julai 7,2020.
Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme Wilaya ya Mpanda Engineer Neema Mushi akisoma taarifa kwa Naibu Waziri alisema,TANESCO wamekusudia kuleta Umeme wa Gridi ya Taifa wenye urefu wa Kilomita 381 unatoka Mkoani Tabora kupitia Mlele hadi Mpanda na lengo ni kufunga mashine Nne lakini kwa kuanzia watafunga Mashine Moja yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 28.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi1QOsRe_KK2GPsybB9MkHn13OKIJSCjcSOJK9bTa_Kbow6VOgDwzQ0HaZjoS2lHOQG-9vX8cYHseK_pwD4OyJc19r1I_WNs6ta2zFiSzHZHZ4M_SZEd-qXg26mYiEBrHYXEW8q7fTnjPo/s640/Engineer+Neema+Mushi%252CMsimamizi+wa+Mradi+wa+Ujenzi+wa+Kituo+cha+Kupoza+Umeme+Wilaya+ya+Mpanda.png)
Engineer Neema Mushi,Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme Wilaya ya Mpanda.
"Nia na madhumuni zitakuwa Nne,kwahiyo tunaanza na Moja hiyo ya Megawati 28,halafu baadaye zitakuja mara Nne yake,na hizi Megawati 28 kwa Mkoa, Mh. pale sisi tumeona wanahitaji Megawati 8,lakini sisi tutakuja na hizo 28 lakini hizi 28 tutakuwa na fida ambayo ndo matoleo zitakuwa 6,Mbili ni kwa ajili ya Viwanda na hizi 4 kwa ajili ya Wananchi"-Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme Wilaya ya Mpanda Engineer Neema Mushi.
Wananchi Kata ya Katumba wakifatilia Hotuba ya Naibu Waziri wa Nishati alipokwenda kuwasha Umeme katika Shule ya Sekondari Kenswa.
Mnamo Tarehe 24,Juni 2020 akitoa mwelekeo wa Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Juma Zuberi Homera katika kikao na Waandishi wa Habari kilichofanyika Ofisini kwake alimuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya CHINA RAILWAY CONSTRUCTION ELECTRIFICATION BUREAU GROUP ( CRCEBG) kwa kutoa Siku 20 ahakikishe anawasha Umeme katika Vijiji vya Karema,Ikola na Kapalamsenga vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,kwa kuwa maeneo hayo ni ya kimkakati.
Comments
Post a Comment