Na Mwandishi Wetu,Site Tv
Dkt.Karist Anthony,Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi,Mwezeshaji wa Mafunzo.Beatrice Matumizi ni Mratibu wa Mradi Elimu Jumuishi Manispaa ya Mpanda, alieleza lengo la wao kutoa mafunzo licha ya maambukizi ya Ugonjwa wa Covid-19 kupungua Nchini ni kutimiza wajibu wao kama Taasisi kwani ana amini si wote wana Elimu ya kutosha.
Mpanda-Katavi.
Watu wenye ulemavu Mkoani Katavi,wamelishukuru kanisa la FPCT kwa kuwapatia mafunzo ya Elimu Jumuishi dhidi ya kujikinga na Virusi vya Corona yaliyotolewa kwa viongozi wanaosimamia watu wenye ulemavu kupitia vyama vyao yaani TAS, CHAVITA, CHAWATA,TLB na TAMS.
Wakizungumza baadhi ya viongozi hao baada ya kupata mafunzo Ndg. Isack Lukas Mlela (Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wasioona Mkoani Katavi (SHIVYAWATA) amesema mafunzo hayo yatawasaidia Watu wenye ulemavu huku akiyashukuru mashirika kwa kuanza kutambua uwepo wa Walemavu na amesema changamoto yao kubwa ilikuwa ni kujua namna ya kujikinga na maradhi hayo.
"Katika Mafunzo haya ya Leo yametusaidia Sana sisi walemavu kuyafahamu ili yaweze kuwasaidia pia familia zetu na wenye ulemavu wengine kutoka katika mafunzo haya kadri ya uelimishaji tutakapofanya huko tunapoishi pamoja na wenzetu,lakini hili ni jambo muafaka kabisa ambalo kweli mashirika yameanza kututambua watu wenye ulemavu,walisahaulika sana katika eneo hili"-Alisema Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Mkoa wa Katavi ambae ni mlevu wa kutoona.
Katibu wa Chama cha TAS Bi. Ashura Shabani amewashukuru Shirika la Elimu Jumuishi kwa kushirikiana na Kanisa la FPCT kwa kuwawezesha Watu wenye ulemavu kupata mafunzo juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Covid-19.
"Nikiwa kama ni mtu mwenye mahitaji maalumu nimefurahi sana,na sisi tutayachukua mafunzo haya tuliyofundishwa kwenda kuwafikishia wenzetu kuwaeleza namna ya kujikinga na ugonjwa huu wa Corona,njia ambazo ugonjwa huu unaenea na hatua gani za kuweza kuchukua,ntawaeleza wanachama wangu wafahamu jinsi ya kujikinga na janga hili"-Alisema Ashura Shabani Katibu TAS.
Ashura Shabani,Katibu wa Chama cha TAS na Mshiriki wa Mafunzo
Kwa upande wake Dkt.Karist Anthony,Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi katika kuwawezesha washiriki amesema,Walemavu ni kundi ambalo limekuwa likisahaulika hasa katika masuala ya Afya hivyo ameiomba Jamii kuwasaidia ili wasiachwe nyuma.
Aidha,alisema zipo njia mbalimbali za kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kunawa Maji tiririka na Sabuni,kutumia vitakasa mikono,kuepuka misongamano sanjari na kuvaa barakoa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_IdHNHE2Cw-73ZWVE7ItrkFjq_OeMLLkwEMeEv-DmENQz8fAIImANtGV8S7A4sRfMgUCHBt9TSHD8a5Te37-9f2A398Su52ncePdpbAbR8HSmw5A_DjuPl1U57_6BfZ3cFoHzP6bwLFo/s640/Screenshot_20200705-201842_2.png)
"Kitu kilichotufanya tuandae mafunzo haya tulikaa na viongozi wa SHIVYAWATA katika kujadili changamoto za Ugonjwa wa Covid-19 kwa watu wenye ulemavu ndipo tulipogundua kuwa kama mradi,Watu wenye ulemavu hawana taarifa za kutosha kuhusiana na Ugonjwa huu,lakini pia hawana uelewa namna ya kuchukua tahadhari"-Beatrice Matumizi,Mratibu wa Mradi Elimu Jumuishi Manispaa ya Mpanda
Bi. Matumizi alisema wao kama Mradi waliweza kugundua Watoto wenye ulemavu wapatao 200 katika Mkoa wa Katavi kwa Mwaka 2018/20.
"Tunafanya kazi hasa na watoto wenye ulemavu kuanzia mwaka 2018-2020 tunao watoto tuliowaibua sisi kama mradi wapatao 200,wapo waliopo shuleni na waliopo majumbani,wengine hali za ulemavu haziwaruhusu kuwepo shuleni ila wale wenye hali zinazowaruhusu kuwepo shuleni wapo shuleni kwaio tuna watoto wanaosoma wapatao 145 kwenye shule hizi zilizopo manispaa ya Mpanda"-Alisema Beatrice Matumizi
Semina hiyo ya siku Moja ilifanyika Julai 4,2020 katika Ofisi za Mradi wa Elimu Jumuishi unaoendeshwa chini ya Kanisa la FPCT,ambapo itakamilika kwa kugawa vifaa mbalimbali kwa Walemavu vikiwemo vya kujinga na Virusi vya Corona.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakichukua umakini kumsikiliza Mwezeshaji.
Comments
Post a Comment