Skip to main content

TASAF KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA TATU YAANZA RASMI UTEKELEZAJI WA AGIZO LA MH.RAIS MAGUFULI

Na Swaum Katambo,Site Tv
Nsimbo-Katavi

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umeanza utekelezaji wa wa kipindi cha Pili cha awamu ya tatu ya TASAF ambapo ruzuku kwa walengwa zitafanyika kwa njia ya Mtandao nchi nzima.

Akitoa Hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wakuu wa Idara na mafunzo ya wawezeshaji wa Halmashauri kuhusu Utekelezaji wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF na uhakiki wa Kaya za walengwa wa Mpango wa kunususru Kaya Masikini uliofanyika katika Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi Josephine Pupia alisema kipindi hiki cha pili kitatekelezwa katika Halmashauri zote 185 za Tanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar.

"Utekelezaji huo utafanyika kwenye Vijiji/Mitaa/Sehia zote nchini na kujumuisha maeneo ya Vijiji/Mitaa/Sehia ambayo hayakupata Fursa hiyo katika kipindi cha kwanza cha utekelezaji wake ambacho kimekamilika."Alisema Bi.Rupia
Kulia (aliyevaa nguo ya kitenge)ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Bi Josephine Pupia kutoka Makao makuu TASAF akiwa kwenye Mafunzo ya Uwezeshaji Nsimbo

Kipindi cha Pili cha awamu ya tatu ya TASAF kitafikia Kaya Milioni Moja na Laki Nne na Nusu zenye jumla ya watu zaidi ya Milioni 7 kote nchini hii ikmiwa ni nyongeza ya Kaya Laki Tatu na Nusu.
"Mkazo Mkubwa katika kipindi cha pili utawekwa katika kuwezesha kaya zitakazoandikishwa kwenye Mpango kufanya kazi ili kuongeza kipato .Aidha kipindi hiki cha Pili kitahakikisha kwamba huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa ili kutoa huduma na kuendeleza rasilimali watoto hususan katika upatikanaji wa Elimu na Afya." Aliongeza Bi Rupia

Kwa upande wake Bw.Deogratius Joachim Dingo ambae ni mwezeshaji katika mafunzo hayo ya kuwajengea uelewa Wakuu wa Idara na wawezeshaji ngazi ya Halmashauri ya Nsimbo alisema Madhumuni ya Mpango katika Kipindi cha Pili ni Kuwezesha kaya za walengwa kutumia fursa za kuongeza kipato na huduma za jamii na uchumi na kuwekeza katika kuendeleza watoto wao,na msisitizo wake ni  Kuwezesha kaya kufanya kazi na hivyo kuongeza kipato,Kuwezesha kaya za walengwa kuongeza rasilimali zalishi na kuongeza vitega uchumi,Kuwekeza katika rasilimali watu hususan watoto ili kuleta matokeo chanya yatakayodumu kwa muda mrefu,Kuboresha upatikanaji wa huduma za maji, afya na elimu, na Kukuza uchumi wa eneo unakofanyika utekelezaji kutokana na matokeo ya Mpango.

"Sehemu Kuu za Mpango kwanza ni Programu za Jamii utafanyika Uhawilishaji fedha zitatolewa ruzuku kwa kaya zenye watoto, kwa  kaya zenye ulemavu na kwa kaya zenye watoto wa kutimiza masharti ya elimu na afya.Miradi ya Kutoa Ajira ya Muda kwa walengwa Muda ikihusisha kuendeleza miundombinu mahsusi ya Afya, Elimu na Maji  pamoja na Kukuza uchumi wa kaya".

"Pili Kuimarisha Taasisi na Mifumo ambapo Uhawilishaji Fedha Utatekelezwa katika Mamlaka za Maeneo ya Utekelezaji zote 187.Ruzuku kwa kaya ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi.Ruzuku kwa kaya zenye watu wenye ulemavu kwa kutambua changamoto na gharama  zinazoongezeka kwa kuishi na mtu mwenye ulemavu.Ruzuku kwa kaya zenye watoto walio shuleni na wale wa chini ya miaka mitano. na Ruzuku kwa kaya kuhawilishwa kwa kwa njia za kielektroniki".Alisema Bw.Dingo
Baadhi ya Wakuu wa Idara wakiwa kwenye mafunzo ya wawezeshaji wa Halmashauri kuhusu Utekelezaji wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF

Miradi ya Kutoa Ajira ya Muda Utekelezaji wake utafanyika kwenye Mamlaka za Maeneo ya Utekelezaji zote 187 ikiwa na Uwiano wa gharama za mradi 75% ujira  na 25% vifaa.Itaangalia vipaumbele vya jamii na itabuniwa kwa njia ya ushirikishwaji wa jamii,Washiriki katika miradi ya ajira ya muda ni wale watakaokuwa na nguvukazi/uwezo wa kutekeleza miradi ya uzalishaji,Mwanakaya mmoja mtu mzima (miaka 18 - 65) mwenye uwezo wa kufanya kazi kutoka kwenye kaya ndiye ataandikishwa kushiriki katika ajira ya muda,Mwanakaya mwingine wa ziada ataandikishwa kushiriki katika ajira ya muda ili kutekeleza miradi endapo mwanakaya mwakilishi hataweza kushiriki kutokana na sababu mbalimbali.

"Miradi ya Kutoa Ajira ya Muda walio katika makundi maalum kama wakinamama wajawazito na wanaonyonyesha au watoto chini ya miaka 18 ambao hawako shuleni watapewa kazi nyepesi na kufanya kazi kwa muda mfupi kuliko wengine,Ujira utakuwa shilingi 3,000 kwa mtu kwa siku,Kaya itashiriki kufanya kazi kwa siku 60 kwa mwaka   ambazo ni siku 10 kwa mwezi kwa miezi sita (6),Muda wa kazi utakuwa saa 4 kwa siku kwa mtu,Kazi zitafanyika kipindi ambacho sio msimu wa kilimo,Ujira utalipwa kwa mwakilishi aliyeandikishwa kutoka kwenye kaya."Aliongeza Bw.Dingo

Miradi ya Kukuza Uchumi wa Kaya Utekelezaji utafanyika katika Mamlaka za Maeneo ya Utekelezaji zote 187 Kaya zote zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi zitashirki kutekeleza miradi ya kuongeza kipato,Walengwa watahamasishwa kuunda vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza na hatimaye kutambulishwa kwenye taasisi za fedha kwa huduma stahiki,Walengwa wataunganishwa na watumishi wa ugani ili kufanya shughuli zao kitaalamu na kwa tija,Elimu za ujasiriamali, stadi za maisha na kujenga fikra na mtazamo chanya zitatolewa  kwa walengwa.
Katika kuimarisha Taasisi na Mifumo itafannyika tathmini ya Mpango,Kuendelea na muundo wa sasa wa utekelezaji,Kuhitimu kutoka kwenye Mpango ikiwa ni pamoja na kuweka mfumo wa kutambua kaya zilizopiga hatua kutoka kwenye umaskini na Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji na kuimarisha Masjala ya Kaya za Walengwa

"Kuimarisha Taasisi na Mifumo,Ushiriki wa walengwa katika Kujenga uelewa wa walengwa kuhusu stahili zao, kuimarisha mfumo wa kushughulikia malalamiko na mifumo ya kuimarisha uwajibikaji.Malipo ya ujira Kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki nchi nzima,Kujenga uwezo Kuimarisha mikutano ya kujenga uelewa wa walengwa, kujenga uwezo wa Kamati za Usimamizi za Jamii na Watumishi wa Ugani,Kufanya uhamasishaji kuhusu masuala ya lishe, uzazi salama na kuimarisha shughuli za kiuchumi,Kujenga uwezo wa Kamati za Usimamizi za Jamii kuhusu manunuzi ngazi ya Jamii na Sera za Kulinda Watu na Mazingira,Kufanya mapitio ya mfumo wa motisha kwa Kamati za Usimamzi za Jamii na Watumishi wa Ugani".Bw Dingo
Mnufaika wa TASAF Nsimbo

Nae Alex Magesa ambaye ndiye Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mpanda Mkoani hapa alisema wanafanya zoezi la Uhakiki wa Kaya Masikini kwa zile kaya zilizokuwa katika Mpango uliopita nia ikiwa ni kuondoa walengwa hewa wakiwemo walengwa waliofariki na walionadili Makazi

"Tunatakiwa tufanye zoezi hilo ndani ya siku tatu tuwe tumeshamaliza kuhakiki watu wote na kuwaweka vizuri majina yao ili tuanze na Mpango mpya wakiingia kusiwepo na kasoro ndogondogo,kwa wale ambao hawajafikiwa sasa hivi kuna zoezi lingine linaendelea kule Vijijini la utambuzi wa awali,watatambuliwa kupitia kwa watendaji wao wa Vijiji watawatambua na watawaorodhesha na wataleta majina yao"Alisema Magessa Mratibu wa TASAF Nsimbo.
Alex Magesa Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi

Ikumbukwe kipindi cha Pili cha awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kilizindiliwa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Mwezi Februali mwaka huu ambapo alizungumzia kuhusu uwepo wa Kaya hewa ambapo alisema

"Uwepo wa Kya hewa katika maeneo ya utekelezaji ni aibu sana kwa viongozi wa Mikoa,Wilaya na Halmashauri.Nitoe woto kwa wahusika wote kusimamia vizuri mradi huu.Serikali haitakuwa na huruma kwa Mtu yeyote,Kufanikiwa ama kutofanikiwa kwenye maeneo yenu itakuwa mojawapo ya vipimonitakavyotumia kujua kama mnastahili kuendelea na nafasimlizonazo au laa,Siwatishi lakini huo ndo ukweli."Mwisho wa kunukuu

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...