SHULE YA SEKONDARI ISACK KAMWELWE YAJA NA MFUMO WA KUTATUA UHABA WA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI,TANESCO KUMALIZA TATIZO LA UMEME KATA YA NSENKWA.
Na Aidan Felson,Site Tv
Mlele,Katavi.
Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Katavi,inatarajia kumaliza tatizo la Umeme kwa kuhakikisha Wananchi wa Kata ya Nsenkwa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mlele wanaunganishiwa Umeme.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu katika ziara yake kikazi ya Siku Mbili Mkoani Katavi,alipokuwa katika Kata hiyo katika zoezi la kuwasha Umeme rasmi katika baadhi ya Kaya katika Kata hiyo.
"Na Mimi naomba nikutaarifu,Vijiji vyako vilivyosalia pamoja na Vitongoji vyake,tunatarajia kupata Wakandarasi Mwezi wa Nane,Mwezi wa Tisa utakapokuja kunadi Ilani ya Uchaguzi ya 2020/2025,we jimwage Mzee kwa raha zako"-Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu akimhakikishia Waziri Kamwelwe kumletea Umeme katika Vijiji vyote vya Kata ya Nsenkwa.
Mh. Mgalu pia amewaomba wawekezaji kuwekeza katika Mkoa wa Katavi kwa kuwa ni Mkoa ambao umefunguliwa na neema imeingia,huku akiwataka Wananchi ambao hawajaunganishiwa Umeme kuwa wavumilivu kwa kuwa zoezi hilo linafanyika kwa awamu.
"Naomba niwaombe wawekezaji wote,Mkoa wa Katavi ni Mkoa ambao umefunguliwa,Mkoa wa Katavi ni Mkoa ambao Neema imeingia,neema ya miundombinu ya Barabara,neema ya Miundombinu ya anga,Mi mwenyewe nimefurahi,nimefika na Ndege hapa"-Mh. Mgalu,Naibu Waziri wa Nishati.
Kwa upnde wake Mbunge wa Jimbo la Katavi na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe alisema Vijiji ambavyo havijapata Umeme ni Mapili,Ilunde,Isegenezya na Masiko na ameishukuru Wizara ya Nishati kwa kukubali kuleta Nguzo 40 katika Kijiji cha Mgombe ambazo zinafika Mwezi ujao.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimlPyHDuyL5GJRmuMMEGe6aXsoxl8S_ljnuwf_FLkjpaG-UpTPYSn_8CWBMx5dgSFRCD19NTrxt58WsnLsFjJSuuKG1ocQoevpZljB-J6H2C9at3pfczZCfGSMElqNmUDtnEGmA__sOsc/s640/Mh.+Kamwelwe.png)
Pichani ni Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu akitoa ufafanuzi kuhusu Mfumo unaofungwa katika Shule ya Sekondari Isack Kamwelwe utakavyokuwa.
Aidha,katika kuhakikisha Nishati inapatikana ili Wanafunzi wapate muda wa kujisomea muda wote,Mh. Kamwelwe amechangia Tsh. Milioni Moja kwa ajili ya kufanya Wiring katika Shule ya Sekondari Isack Kamwelwe,na alisema hadi sasa Shule hiyo inafungwa Mtambo wa Teleconference utakao tatua tatizo la ukosefu wa Walimu wa Masomo ya Sayansi kwa kuwa Mfumo huo utaunganishwa na Walimu wa masomo hayo.
"Huyu Bwana (Meneja wa TTCL) ndiye anayetuletea Teleconference hapa,ameshanunua vifaa vyote,na ile Optic fiber amenunua,ilikuwa wafunge upande wa TANESCO lakini sasa conectivity ime fail,kwasababu lazima tuje na hii Barabara ya Lami,kwahiyo wanaleta nguzo 150,ukikamilika tunafunga sceen hapa,tunaanza kufanya E-Education,kwahiyo itaondoa changamoto ya Walimu wa Sayansi hawapo,Walimu wa Hesabu hawapo,Moja tutaunganisha na Dar Es Salaam Institute Of Technology"-Mhandisi Kamwelwe,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiy0P60vL1oKaUdYD0lZkED_z9p6qlaykVyjx8Zu24LFwCfU40Y-smLwhw843LXilGAsE6CYGbJAJ61hP3SZeawHGBYX0taSs8dN_VTVqanqyKH-mdJuLa42w0-MjxukftRr6pxNXn1TdE/s640/Kamwelwe.png)
Pichani ni Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu akiwa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe wakifurahia jambo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhr6YTH2Lq6ou82FPdNZuQr7NURv9WSaJxc1ADSBrDiwD7cJhq3C_di0b05rGm4fs-hfxrtQ7EVjB8GZq1BQ6u3s8TOtSkkq_nD-x7deaYKXCwWgOqOwbjVDFQpQxA2SsYdFy4uLV8UB5A/s640/Wanafunzi.png)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLhc1Cm9ppC7y8FEDx7AXFtCb64Hm_w1TOh4pILtisGnMuEdz8ZZX_PTdqW3NFOzp676LZyzr9BCYRpDdX4PVjM1CeNWWKBBjzaWCPJwkJG0qYxM3zEiZwzCbCmVfVMVhh787i4hlfKnc/s640/vlcsnap-2020-07-08-12h58m54s110.png)
Comments
Post a Comment