Skip to main content

Serikali yatoa bilioni 16 kutekeleza miradi ya maji Ruvuma

Miradi ya maji wilaya ya Nyasa

SERIKALI ya awamu ya tano imetoa zaidi ya shilingi bilioni 16 kutekeleza miradi mbalimbali ya maji mkoani Ruvuma hali iliyoweza wananchi 1,149,867 kupata maji safi na salama hadi kufikia mwakahuu.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema idadi ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi na salama katika Mkoa wa Ruvuma hivi sasa ni asilimia 63.9 ya wakazi wote wa Mkoa idadi ambayo imeongezeka kutoka asilimia 57 ya wananchi waliokuwa wakipata huduma
hiyo mwaka 2015.

Hata hivyo Mndeme amewataja wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini wanaopata huduma ya maji safi na salama wanakadiriwa kuwa 888,005 ambao ni sawa na asilimia 61.6,ambao wanapata maji kupitia vituo vyakuchotea maji 5,631 .

“Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama na kufikia malengo ya kitaifa, Mhe, Rais ameendelea kuwezesha ukarabati na ujenzi wa miradi mipya ya maji, kuanzisha na kusajili kisheria jumuiya za watumia maji vijijini kwa ajili ya kusimamia na kuendesha miradi ya
maji’’,alisema.
Miradi ya maji wilaya ya Songea

Kuhusu huduma ya maji mijini,Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa wa Ruvuma una miji sita ambayo ni makao makuu ya Halmashauri ukiwepo mji wa Songea ambao ni makao makuu ya Mkoa. Miji hiyo ni Songea, Mbinga, Tunduru, Namtumbo, Mbambabay na Madaba.

Mndeme amesema Hadi kufikia mwaka 2020 hupatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Manispaa ya Songea umefikia asilimia 91 ikilinganishwa na asilimia 72.7 kwa mwaka 2015.

Ameutaja Mpango wa utekelezaji miradi ya maji vijijini katika mwaka wa fedha 2019/2020,serikali imeupatia Mkoa wa Ruvuma kiasi cha shilingi 1,168,888,500.83 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa miradi 29 ya maji.

Mndeme amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2020,serikali imeupatia Mkoa wa Ruvuma shilingi bilioni 7.8 kwa ajili ya Kujenga, kukarabati na kufanya upanuzi katika miradi 33 ya maji katika wilaya zote tano .

Akizungumzia hali ya utekelezaji wa miradi kupitia programu ya lipa kwa matokeo na Mfuko wa Maji,Mkuu wa Mkoa amesema hadi kufikia mwaka 2020 Kupitia Program ya lipa kwa matokeo , Jumla ya miradi 19 imekamilika,miradi kumi inaendelea kutekelezwa na miradi 33 iko kwenye
hatua mbalimbali za utekelezaji.

Ameongeza kuwa katika kukabiliana na tatizo la maji, Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu ya maji na kupanua mitandao ya maji ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akikagua mradi wa maji katika kijiji cha Chimate wilaya ya Nyasa

Maelekezo ya Ilani ya CCM ya mwaka 2015 ni kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama vijijini unaongezeka toka asilimia 67.7 mwaka 2015 na kufikia asilimia 85 mwaka 2020; miji ya makao makuu ya Mikoa toka asilimia 68 mwaka 2015 na kufikia asilimia 95 mwaka 2020 na miji mikuu ya Wilaya na miji midogo toka asilimia 57 mwaka 2015 hadi asilimia 90 mwaka 2020.


Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...