Skip to main content

MRADI WA MITI KUKIINGIZIA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA MBIFACU MILIONI 553

Chama kikuu cha ushirika MBIFACU mjini Mbinga

CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Wilaya za Mbinga na Nyasa(MBIFACU) kimeanzisha shamba la miti la Kitelea mjini Mbinga lenye ukubwa wa hekari 39 lililopo kando kando ya barabara iendayo Mbambabay wilayani Nyasa.

Kaimu Meneja wa MBIFACU Henrick Ndimbo amesema chama hicho kimeanzisha shamba hilo kwa lengo la kujiongezea mapato na kuimarisha ushirika kutokana na maelekezo ya serikali ya awamu ya
Tano yenye lengo la kufufua ushirika nchini.

Ndimbo amesema kupitia shamba hilo,katika msimu wa mwaka 2019/2020 MBIFACU imefanikiwa kuuza miti 118 yenye thamani ya shilingi 2,360,000/= na kwamba fedha hizo ziliingizwa kwenye mapato ya chama ili kuweza kusaidia uendeshaji wa shughuli mbalimbali za
chama.

“Mpango mkakati wa mwaka 2020/2021 ni uvunaji wa miti kwa hekari 30 na uchanaji wa mbao ambazo zinatarajia kutuingizia kipato cha shilingi milioni 553,630,000/= baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji,ikiwa ni moja ya juhudi za kuongeza mapato ya ndani ya chama ili kiweze kujitegemea’’,alisisitiza Ndimbo.

Ndimbo ametoa rai kwa Taasisi zote kushirikiana na MBIFACU katika kutekeleza na kusimamia mfumo wa ushirika kwa sababu ndiyo mkombozi wa wakulima ambao unaweza kuwanufaisha wakulima,endapo mfumo wa ushirika utasimamiwa vizuri kupitia wataalam.

Amesisitiza kuwa ushirika utaongeza uzalishaji kwa kuongeza kipato cha wakulima moja kwa moja na kuongeza mapato ya Halmashauri ya serikali kwa ujumla.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa MBIFACU Winfred Lupembe
amesema shamba la miti la Kitelea ni la miti ya zamani ambapo MBIFACU imeamua kuliboresha shamba hilo kwa kuvuna miti yote kwamatumizi ya mbao na kuni na kwamba baada ya kukamilisha kazi yakuvuna,MBIFACU inatarajia kupanda miti upya kibiashara na kuingiza mapato makubwa zaidi.

Lupembe amesisitiza kuwa zoezi la uvunaji miti ya zamani na kupanda miti mipya linaendelea ambapo katika eneo hilo tayari imepandwa mitimipya 600 na kwamba shamba la miti linalomilikiwa na MBIFACU,ukitembea kwa mguu unaweza kutembea kwa saa mbili na nusu kuzunguka shamba lote.
Sehemu ya miti katika shamba la miti Kitelea Mbinga lenye ukubwa wa hekari 39 linalomilikiwa na MBIFACU

Amesema miti yote ambayo ilipandwa katika shamba la miti la Kitelea ilishavunwa na kwamba miti iliyopo hivi sasa ni michipukizi ya miti zamani ambayo pia inavunwa kwa ajili ya mbao za kuendeleza mradi wa ukarabati wa hoteli ya MBICU kuwa katika viwango vya kimataifa.

Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja