Skip to main content

HALMASHAURI YA MJI MBINGA ILIVYOFANIKIWA KUJENGA NYUMBA NANE ZA WATUMISHI KWA MILIONI 650

Mradi wa nyumba saba za wakuu wa Idara wenye thamani ya shilingi milioni 350 ambao unatekelezwa katika Halmashauri ya Mji Mbinga,ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 75

HALMASHAURI ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma, imetumia shilingi milioni 650 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba saba za wakuu wa Idara na nyumba moja ya Mkurugenzi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Grace Quintine amesema Halmashauri yake katika kipindi cha mwaka 2019/2020 ilipokea kiasi cha sh.milioni 350 kwa ajili ya nyumba saba za wakuu wa Idara na kwamba shughuli za utekelezaji zilianza Machi 26 ambapo hadi sasa
mradi umefikia asilimia 75.

“Jumla ya shilingi milioni 284.374 zimetumika hadi sasa kati ya milioni 350,vifaa vyote vya viwandani kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo vimenunuliwa’’,alisema Quintine.

Amesema mradi ulitarajiwa kukamilika Juni mwaka huu,hata hivyo kutokana na changamoto ya kuchelewa kupokea bati ambazo ziliagizwamoja kwa moja kiwandani ALAF ilisababisha mradi kusimama kwa wiki mbili ambapo sasa mradi unatarajia kukamilika mwishoni mwa Julai
mwaka huu.

Amesema miradi yote miwili inatekelezwa kwa kutumia force account ambapo kuna kamati tatu zinazosimamia mradi huu ikiwemo kamati ya ujenzi,kamati ya manunuzi na kamati ya mapokezi na ukaguzi.

Akizungumzia mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi,Quintine amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2020 Halmashauri iliidhinishiwa kutumia milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya
Mkurugenzi ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 65.

Amesema mradi huo pia unatekelezwa kwa force account na kwamba licha ya changamoto zilizochelewa mradi,hadi kufikia mwishoni mwa Julai mwaka huu,mradi wa nyumba ya Mkurugenzi unatarajia kukamilika kwa asilimia 100.

Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Musa Homera ilikagua miradi yote miwili na kuridhishwa na utekelezaji wake ambao unakwenda kuondoa changamoto ya nyumba za kuishi kwa wakuu wa Idara na Mkurugenzi
katika Halmashauri ya Mji Mbinga.

Homera ametoa rai kwa Halmashauri nyingine za Mkoa wa Ruvuma kuiga mfano wa Halmashauri hiyo ambapo sasa serikali itaondokana na kuwalipia wakuu wa Idara posho ya nyumba na fedha hizo kutumika katika shughuli nyingine za kuwaletea maendeleo wananchi wa Mbinga.

Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja