Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti Dawa za Kulevya Kanali Burhan Nassor. Na Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 E-mail: abdya062@gmail.com RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema wakati umefika wa Wazanzibari kuungana pamoja katika vita dhidi ya usafirishaji na matumizi ya Dawa za kulevya pamoja na kuvitaka vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanyakazi kwa weledi na ufanisi. Dk. Mwinyi ametoa rai hiyo leo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya kupinga matumizi na Usafirishaji wa Dawa za Kulevya Duniani, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Jijini Zanzibar. Amesema ili kufanikisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya kuna umuhimu wa jamii kuungana, huku akivitaka Vyombo vya Ulinzi na Usamala pamoja na taasisi nyengine zinazohusika na mapambano hayo,ikiwemo Jeshi la Polisi, Mahakama na Ofisi ya Mkemia Mkuu kufanyakazi kwa misingi ya sheria...