Skip to main content

Wilaya ya Nyasa yatoa mikopo kwa Asilimia 100,RC Ibuge apongeza.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akizungumza katika mkutano maalum wa CAG Halmashauri ya wilaya ya Nyasa katika ukumbi wa Kapteni Komba mjini Mbambabay.


Na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali  Wilbert Ibuge,ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa kutoa mikopo kwa asilimia 100  yenye thamani ya ya zaidi ya shilingi milioni 66.6 kwa  makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

RC Ibuge ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki katika mkutano maalum wa Baraza la madiwani la Halmashauri hiyo wa kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa mwaka 2019/2020.

Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Kepteni John Komba mjini Mbambabay Makao makuu ya Wilaya ya Nyasa.

Brigedia Jenerali Ibuge amepongeza mara ya kwanza Halmashauri hiyo kutoa mikopo kwa asilimia 100 ambapo kati ya fedha zilizotolewa Wanawake wamepata milioni 37.6 vijana, milioni 19,000,000 kundi la watu wenye ulemavu shilingi milioni 10,000,000.

Katika hatua nyingine RC Ibuge ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kufanikiwa kukusanya mapato ya ndani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.2 ambayo ni sawa na  asilimia 82.95.

“Kwa moyo wa dhati kabisa naipongeza Halmashauri hii kwa kutoa mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kuwa makundi hayo ni muhimu katika Uzalishaji mali”,alisisitiza RC Ibuge.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewaagiza Madiwani na watendaji wa Halmashauri kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kuinua makusanyo na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa asilimia 100.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mhe.Stewart Nombo ameahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja