![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEit_U-lDAZciAkhVoGcsr6saOqEOqvXyNdHMbujeVdeGHUuwL20qvOuyY0Mcb1lYRoT-eoO3ZwMz9kRfG0ZM21htm1LbEu68Zhjee2hf5PEWwCvyd_1NFx_Uz-1zAXEHTcqgsmduqMepfU/w640-h360/vlcsnap-2021-06-15-17h55m45s662.png)
Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika,Salehe Mhando (aliyevaa Suti) akiwa na baadhi ya Wakulima wa Pamba katika tukio la uzinduzi wa Soko la Pamba katika Kijiji cha Sibwesa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiIRT1hZb8Bj3aWt_0NMfGn8eDKVvHLcELlApSu5h-dPSbGgdKPgX64K0BcKfxLkWmdlAGlwSxkfgvLLR7nm6qAQIImbYqE3ZNACN8gKD3ywm4w-9DkSvX-63KDn9RiZaBItYSIU1C_5lc/w640-h360/vlcsnap-2021-06-15-17h55m22s856.png)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4VOtYh9KNFAbNvcuqLuRrPlurUQPPzhuIkSh8sFERn5qrGLSHo6PR0Rv5p4qlnecAiIXqJYjWYWiehM5kpy46TpD1p5ziamZteh3V5tpj0lhUIlfROJjwcTpcfA1NIEG35G-6tuZE7Kg/w640-h360/vlcsnap-2021-06-15-17h56m05s694.png)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGsFVhFBdtbtOhPwP-RY10zXDHAZTu4r6dDXsloKJrHNwRlPlkgKhedT40cgVQRaO38wrvWQFZb6E9PAz0uOEgAYsiBEE9rFIDb4RrJBSdGa_0LjLDX-QnA22tO3aKhB8wZmMcpP9BzpM/w640-h360/vlcsnap-2021-06-15-17h56m36s309.png)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSkNGzxAkqUYP59KOJerLdYtlYAoN1nUZK0vmHmQFkgdpgVvkwo7WFJkp4MjupZQHEgiCU1_9K53vJkIBZwhueiHsYcea5seh7dUd4kVahaeiM8dOwLX9iJDi0jCidOKoQ7XnXWq7Pbzk/w640-h360/vlcsnap-2021-06-15-17h52m02s865.png)
Mnunuzi wa Pamba kutoka Kampuni ya NGS Investment Co.Ltd Njalu Daudi Silanga.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgALXQzkhLG4nkoyRt2TVJuvxqqkvMDYAq_k8FbgphH4ORNJgi2K1t29jxkab0LEIDhwv56MjUl_WN25Ksd9uMZkhyphenhyphenlsU317VbLlYwWXTjOhfupYxZPIC4Q-mekSw3MHR8maFyfm2YHzy8/w640-h360/vlcsnap-2021-06-15-17h57m23s316.png)
Pichani ni Sephania Waya kutoka Idara ya Kilimo Wilayani Tanganyika.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkkTWyer-jL213FCM0A6FH16-8YhKgK_Cm2OfVgaSxfvwXBcgbDn5XdkgSJlMtsMsZd3lQKh6j3EzCgbjxSnrefUNshRxKSehs1E-5rrTYro90RyKvRRtPS_0F9SjThiLSzCgWPC0QiLo/w640-h360/vlcsnap-2021-06-15-17h52m52s190.png)
Na.Swaum Katambo
Tanganyika-Katavi.
Wakulima wa Pamba Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi wameipongeza Serikali kwa usimamizi mzuri wa ununuzi wa Pamba kwa bei elekezi ya Sh.1050 ukilinganisha na mwaka jana ambapo waliuza kwa Sh.810.
Wakizungumza katika tukio la uzinduzi wa Soko la Pamba uliofanyika Jana Juni 15,2021 katika Kijiji cha Sibwesa Wilayani humo,Wakulima wamesema kuwa mwaka huu wamepata manufaa ukilinganisha na gharama za uandaaji wa mashamba,ununuzi wa mbegu pamoja na palizi.
"Mwaka wa kwanza wakati wanzindua Pamba walikuwa wananunua kwa bei ya sh 1200 lakini kwenye malipo wananchi walidhurumika,hiyo ilipelekea kwenda kupungua kwa uzalishaji wa zao la Pamba"Alisema Kusekwa Mathias
Hata hivyo pamoja na unafuu wa kuongezeka kwa Bei elekezi ya mwaka huu Wakulima pia wameiomba Serikali kuangalia tena suala la bei ya Pamba kwani gharama za Uzalishaji ni kubwa hivyo faida wanayoipata ni ndogo.
Nae Mnunuzi wa Pamba kutoka Kampuni ya NGS Investment Co.Ltd Njalu Daudi Silanga amesema pamoja na kuwa wao ni wanunuzi wa Pamba lakini wataendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Makarani ili kujua nini kinaendelea kwenye maeneo yao na kusema kuwa kazi hiyo si ya Serikali pekee.
"Kama kununua Pamba hakuna anayenizidi hapa,nimeanza kununua Pamba kwa Sandarusi,na mtu anaposema kwamba amekula shoti sio amekula shoti amebeba zile hela",alisema Njalu Silanga Mnunuzi wa Pamba.
Kwa upande wake Sephania Waya kutoka Idara ya Kilimo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halimashauri ya Wilaya ya Tanganyika amesema kwa Msimu wa Kilimo 2020/21 zilijitokeza changamoto mbalimbali ikiwemo Wakulima wengi kutokuwa na Elimu ya Kanuni za Kilimo bora cha Pamba na Matumizi sahihi ya Viuatilifu na Vinyunyizi hivyo ili kukabiliana na changamoto hiyo wamepanga kutoa Elimu ya utambuzi,uthibiti wa wadudu waharibifu na matumizi sahihi ya Viuatilifu na Vinyunyizi kwa wakulima kupitia Mikutano ya Wakulima na Redio za Kijamii.
Nae Mgeni rasmi katika tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando amesema hatarajii kusikia mkulima hata mmoja analalamika kutolipwa pesa yake hivyo ametoa maagizo kwa Afisa Kilimo,watendaji na Maafisa Tarafa,wenyeviti,Madiwani na Bodi za Amcos kwa Wilaya nzima.
"Makarani najua Mikataba yenu haitazidi zaidi ya Miezi miwili sitatarajia kumuona Karani baada ya Miezi hii miwili anamiliki Gari..,ameenda kununua kundi la Ng'ombe,taarifa hizo zilikuwa zinafanyika hapa ninazo"-Alisema DC Mhando
MWISHO.
Comments
Post a Comment