Skip to main content

RC IBUGE akagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji kupitia Ziwa Nyasa.


Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma na Kamati ya Ulinzi  na Usalama wilaya ya Nyasa,wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali ndani ya Mto Chiwindi ambao unagawa nchi ya Tanzania na Msumbiji kupitia wilaya ya Nyasa


Ni mmoja wa askari kutoka nchi ya Msumbiji akiwa  ng'ambo ya Mto Chiwindi ambako ni kijiji cha Shiwindi nchini Msumbiji akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge alipofanya ziara ya kutembelea mpaka wa Chiwindi unaotenganisha Tanzania na Msumbiji.


Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akizungumza na viongozi wa serikali katika ,kijiji cha Chiwindi Kata ya Chiwanda wilayani Nyasa,mpakani mwa Tanzania na nchi ya Msumbuji.


Na.Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amefanya ziara ya pili ya kukagua maeneo ya mipakani kwa kutembelea mpaka wa Chiwindi mwambao mwa ziwa Nyasa unaogawa Tanzania na nchi ya Msumbiji.

RC Ibuge katika ziara hiyo aliongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Nyasa.

Akizungumza na viongozi na watendaji wa serikali katika kijiji cha Chiwindi,wilayani Nyasa,RC Ibuge ameagiza ulinzi na usalama katika eneo la mpaka kuimarishwa zaidi ili wananchi wanaoishi mpakani wasiwe na hofu bali waendelee kushiriki katika kazi za uzalishaji mali.

Hata hivyo amewataka wananchi wanaoishi mpakani kuwa walinzi wa kwanza na endapo wataona dalili za hatari wasipuuze, bali watoa taarifa haraka katika ngazi za juu ili hatua zichukuliwe haraka.

Ametoa rai kwa wananchi na wafanyabiashara wanaovuka mpaka kwenda Msumbiji kufuata maelekezo ya serikali,na hasa kutokana na kile ambacho kinaendelea katika nchi ya Msumbiji vikiwemo vitendo vya ugaidi ambapo amesisitiza kipaumbele cha kwanza kiwe ni maslahi ya Taifa.

Amewatahadharisha viongozi na watendaji waliopo mpakani wasiruhusu vitendo ambavyo vinahatarisha amani katika mipaka ya nchi ukiwemo mpaka wa Chiwindi ambako kuna mwingiliano wa wageni kutoka Msumbiji na kuingia Tanzania.

“Mipango ya serikali ni mikubwa,Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ana lengo la kuiendeleza nchi hii ipige hatua kubwa katika maendeleo’’,alisisitiza RC Ibuge.

Hata hivyo amesema bila amani na utulivu hakuna maendeleo,ambapo amewapongeza wananchi mwambao mwa ziwa kwa kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo cha zao la muhogo.

Hata hivyo amesema serikali kupitia ngazi ya wilaya ya Nyasa, inaandaa mpango kuviwezesha vikundi vidogo ili viweze kufanya kilimo cha ziada cha kuongeza kipato ambapo amesema wilaya ya Nyasa inafaa kwa kilimo cha michikichi ambacho kinazalisha mafuta ya kula ambayo yana soko kubwa hapa nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa ziara hiyo,ambayo amesema imeleta faraja kubwa kwa wananchi wa kijiji cha Chiwindi kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Hii ni ziara ya pili ya RC Ibuge kukagua maeneo ya mipaka katika Mkoa wa Ruvuma,ambapo katika ziara ya kwanza RC Ibuge alikagua mpaka wa Mkenda unaoigawa Tanzania na Msumbiji kupitia Mto Ruvuma wilaya ya Songea.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja