Skip to main content

Wakulima Morogoro wanufaika na Mradi wa zao la Mpunga.


Picha ikionesha Mfereji mkuu unaoepeleka maji mashambani katika skimu ya Msolwa Ujamaa.


Sehemu ya Miundombinu katika skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji Msolwa ujamaa Kilosa mkoani Morogoro.


Picha Ikionesha Ghala la kuifadhia mazao katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Njage katika Halmashauri ya Mlimba.


Bi. Wadara Kitada Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Mlimba Mkoani Morogoro akizungumza katika skimu ya Njage wakati wa ziara ya kikazi katika miradi ya kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga.

Na. Mwandhishi Wetu-Morogoro.

Wakulima katika skimu za kilimo cha umwagiliaji Mvumi, Msolwa Ujamaa na Njage zilizopo katika Wilaya ya Kilosa, Kilombero na Halmashauri ya Mlimba Mkoani Morogoro, zimenufaika na ukamilishwaji wa ujenzi wa skimu za kilimo cha umwagiliaji zilizopo chini ya mradi wa kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga uliyofadhiliwa na Bank ya Dunia.

Wakiongea katika nyakati tofauti baadhi ya wakulima katika skimu hizo,walisema hali ya kilimo katika skimu hizo haikuwa rafiki kabla ya kuwepo kwa ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo kwa sasa, hali ya kilimo ni nzuri kwani kuna uhakika wa kupata wastani wa mavuno ya gunia 20 mpaka 30 kwa heka kutokana na uhakika na matumizi sahihi ya maji katika misimu tofauti ya kilimo.

Bi Mwanaisha Kaluwa mkulima katika Skimu aya Mvumi Wilayani kilosa amesema “Naishukuru Serikali kwa kushirikiana na Bank ya Dunia kwa kutuletea mradi wenye manufaa kwetu sisi wakulima lakini Ombi langu ni kwamba Serikali itutaftie masoko ya uhakika kwani kwa sasa tunauza kupitia madalali ambao wanatuumiza sana , hawatumii vifungashio halali wanafunga kwa ktumia umbesa, tunaomba sana Serikali isimamie mpunga uuzwe kwa kutumia mizani.” Alisema Bi. Mwanaisha.

Afisa kilimo wa Halmashauri ya Mlimba Bi Wadara Kidata, akiongelea skimu ya kilimo cha umwagiliaji Njage alisema kabla ya mradi skimu ilikuwa na changamoto ya maji ambayo kwa sasa wanapata maji kwa wakati barabara ni nzuri ambazo zinarahisisha mazao kufika ghalani na kwa wanunuzi kwa wakati na gharama nafuu.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mhandisi wa mkoa wa Umwagiliaji Morogoro Njanji Mlole, alisema kabla ya kukabidhi mradi huo ambao upo katika muda wa matazamio, mapungufu machache yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na kurekebisha mabanio na kuinua sehemu ya vipange vya barabara za skimu na kubadilisha ma karavati katika skimu ya Njage Mlimba, pamoja na kuingiza mfumo wa maji safi katika vyoo yatarekebishwa katika kipindi hicho kwa mujibu wa mkataba.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja