Skip to main content

Wazee wa Mkoa wa Ruvuma waunda Baraza la Wazee.

Wawakilishi wa wazee wa Mkoa wa Ruvuma kutoka wilaya  zote tano wakiwa katika kikao maalum cha kuunda Baraza la wazee wa Mkoa pamoja na kuchagua viongozi watakaoongoza Baraza hilo ngazi ya Mkoa wa Ruvuma.


Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu akifungua kikao maalum cha uundaji wa Baraza la wazee Mkoa wa Ruvuma na kufanya  uchaguzi wa kuwapata viongozi watakaoliongoza baraza hilo ngazi ya Mkoa.

Na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Wazee wa Mkoa wa Ruvuma wamefanya kikao maalum cha uundaji Baraza la Wazee la Mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mipango Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea.

Waliochaguliwa kuunda Baraza hilo kwenye uchaguzi ulishirikisha wawakilishi kutoka wilaya za Nyasa,Mbinga,Songea,Tunduru na Namtumbo ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa amechaguliwa Elenzian Nyoni kutoka Manispaa ya Songea.

Wengine waliochaguliwa ni Lusiana Nduguru kutoka Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambaye amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti,Katibu ni Winfrid Mbilinyi kutoka Halmashauri ya Madaba na Naibu Katibu Philipo Katyale kutoka Halmashauri ya Songea.

Viongozi wengine waliochaguliwa kuunda Baraza la Wazee wa Mkoa ni Mtunza Hazina amechaguliwa Esta Nzuyu kutoka Halmashauri ya Mji wa Mbinga,Mwakilishi wa wanaume Yustin Mande kutoka Halmashauri ya Nyasa na Mwakilishi wa wanawake amechaguliwa Maria Luoga kutoka Manispaa ya Songea.

Akizungumza wakati anafungua kikao cha uchaguzi huo,mgeni rasmi Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bakari Ally Mketo amesema Taifa linawategemea sana wazee ambao ni hazina kubwa katika jamii.

“Taifa bila wazee halina dira,wala muelekeo,sehemu yeyote panapokosekana wazee,pana hatari ya kuangamia’’,alisisitiza Mketo.

Amesema vijana wana mengi ya kujifunza kutoka kwa wazee kwa sababu wazee wanafahamu siri kubwa na hekima ya kuwa kiongozi bora ambapo amesisitiza kuwa Taifa linawategemea wazee ndiyo maana yanaundwa mabaraza ya wazee katika ngazi mbalimbali.

Amesema serikali imetoa nguvu kubwa katika mabaraza ya wazee na kwamba busara ya wazee kwenye mabaraza hayo itasaidia kutafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja