Skip to main content

RC Ruvuma akabidhi Vifaa maalum vya utoaji Elimu dhidi ya Corona.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimkabidhi vifaa maalum kwa kutolea elimu dhidi ya Corona Mkuu mpya wa Wilaya ya Mbinga Mhe.Aziza Ally Mangasonga.


Mkuu wa wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimkabidhi vifaa maalum kwa kutolea elimu dhidi ya Corona Mkuu mpya wa  wilaya ya Namtumbo Mhe.Julius Keneth Ningu.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimkabidhi vifaa maalum vya kutolea elimu dhidi ya Corona mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimkabidhi vifaa maalum vya kutolea elimu dhidi ya Corona kwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Elias Thomas.

Na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewakabidhi wakuu wa wilaya watano vipaza sauti kwa ajili ya utoaji wa elimu kwa jamii ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

RC Ibuge amekabidhi vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea.

Amewaagiza wakuu wa wilaya wanapokwenda kwenye maeneo yao ya kazi,kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kuendelea kuwahamasisha wananchi kujikinga na kuchukua hatua zinazostahiki dhidi ya ugonjwa wa homa kali mapafu yaani UVICO-19.

Akizungumza baada ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,vifaa vya kutolea elimu dhidi ya corona,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dr.Jairy Kanga amesema Dunia hivi sasa ipo katika mapambano makali dhidi ya UVICO-19 hivyo elimu endelevu inatakiwa kutolewa kwa wananchi.

Ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo corona kwa kuvaa barokoa wanapokuwa kwenye mikusanyiko na ametoa rai kujiepusha na misongomano isiyokuwa ya lazima.

“Kila inavyowezekana tutumie vipukusa mikono (sanitizer),njia rahisi na salama zaidi kwa wananchi ni kunawa mikono kwa kutumia maji yanayotiririka kwa kutumia sabuni,naamini kila Mtanzania ana sabuni’’,alisisitiza.

Hata hivyo amelitaja jambo muhimu katika kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza ni kufanya mazoezi kwa sababu mazoezi yanaamsha kinga za mwili na kufanya mtu kuwa na kinga bora hivyo kuepukana na magonjwa ya kuambukiza.

Mganga Mkuu huyo wa Mkoa wa Ruvuma amesema kuna viashiria vya kuingia wimbi la tatu la corona hapa nchini ambapo tayari nchi jirani zetu kama Kenya wameingia kwenye wimbi la tatu,hivyo amesisitiza ni vema kuchukua tahadhari,ingawa amesema hadi sasa katika Mkoa wa Ruvuma hakuna mgonjwa wa corona.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja

Katavi Yakemea Vikali Ushoga,Mauaji "Wanaume Msiwazuie Wake Zenu Kufanya...