Skip to main content

Fedha za Ushuru Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kuchunguzwa.







Mkaguzi wa nje wa hesabu za Serikali Mkoa wa Katavi,Mohamed Msangi akieleza jambo katika Mkutano wa Baraza la hoja la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.


Na. Zainab Mtima,

Tanganyika-Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Bi. Mwanamvua Mrindoko ameagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoania humo, kufatilia fedha zote za ushuru zilizotumiwa kinyume na utaratibu kabla ya fedha hizo hazijaingizwa kwenye mfumo.

Mrindoko ametoa maagizo hayo katika mkutano wa baraza la hoja la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ambapo amesema serikali haiwezi kuvumilia wizi wa aina hiyo ya matumizi holela ya fedha za serikali ambazohazijaingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.

Pia amemtaka mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Bwana. Hamadi Mapengo kuhakikisha anasimamia hoja zote 35 zilizosalia kati ya hoja 55 zilizotolewa na mdhibiti na mkaguzi wa nje wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka 2019-2020 zinafungwa haraka iwezekanavyo.

Miongoni mwa hoja hizo ni pamoja na madeni ya halmashauri pamoja na matumizi mabaya ya fedha za ushuru.

Sambamba na hilo Mrindoko amesema suala ya hoja kujirudia kila mwaka ni uzembe na kutowajibika kwa watumishi ipasavyo.

Kwa upande wake mkaguzi wa nje wa hesabu za serikali mkoa, Mohamed Msangi amesema hoja zilizojibiwa ni asilimia 36 pekee, huku asilimia 64 ya hoja zikiwa bado hazijapata majibu, huku fedha za serikali zikionekana kutumiwa ndivyo sivyo.

Katika hatua nyingine Mrindoko amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na Katibu Tawala wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia suala la watumishi hewa ili kuepuka mianya ya malipo hewa kwa watumishi ambao tayari wamehamishwa.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja

Katavi Yakemea Vikali Ushoga,Mauaji "Wanaume Msiwazuie Wake Zenu Kufanya...