Skip to main content

Wahudumu wa kujitolea Ruvuma wapewa msaada wa Baiskeli 15.


Miongoni mwa wahudumu wa kujitolea mkoani Ruvuma waliopewa msaada wa baiskeli 15 kutoka kutoka shirika la SATFkupitia ubalozi wa Marekani.


Katikati ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema akikata utepe kuzindua baskeli 15 zilizotolewa na ubalozi wa Marekani kwa wahudumu wa kujitolea Mkoa wa Ruvuma.

Na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Wahudumu 15 wa kujitolea ngazi ya Jamii ambao wamekuwa wanafanyakazi ya kuwasaidia watoto wa kaya masikini 423 mkoani Ruvuma wamepewa msaada wa baiskeli ili kuwasaidia kutoa huduma kwa jamii.

Msaada huo umetolewa na Shirika la Social Action Trust Fund(SATF) kwa udhamini wa mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI(PEPFAR), kupitia mfuko wa Balozi wa Marekani nchini Tanzania.

Akitoa taarifa kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea ,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa SATF Dkt.Sylivia Ruambo amesema jumla ya shilingi milioni 3.7 zimetumika kununua na kusafirisha baskeli hizo hadi Songea.

Dkt.Ruambo amebainisha kuwa SATF inatekeleza mradi wa tuwalinde watoto katika Halmashauri tatu za Mkoa wa Ruvuma ambazo amezitaja kuwa ni Madaba,Songea na Nyasa na kwamba mradi huo ni wa mwaka mmoja.

“Mradi umelenga kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata huduma za elimu,afya,ulinzi na haki za mtoto pamoja na kuziwezesha kaya masikini kujenga uwezo kiuchumi’’,alisisitiza Dkt.Ruambo.

Hata hivyo amesema,pamoja na shughuli nyingine,mradi huo uliwajengea uwezo wahudumu 15 wa kujitolea katika ngazi ya Kata ambao wamekuwa wanasaidia kuielimisha jamii kuhusu haki za mtoto na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Amesema,mradi umeamua kuwanunulia basikeli wahudumu hao ili kuwarahisishia usafiri na kuwafikia walengwa majumbani kwao.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi basikeli hizo,Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema ametoa rai kwa wahudumu hao kuzitunza basikeli hizo na kuendelea kuwatumikia walengwa kama mradi ulivyoelekeza.

“Natambua kazi yenu kwa sehemu kubwa ni ya kujitolea,hivyo nawaomba mtangulize mbele maslahi ya jamii ili kuweza kutimiza adhima ya kuwahudumia’’,alisisitiza Mgema.

Mgema amelishukuru Shirika la SATF na PEPFAR kupitia ubalozi wa Marekani kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya mkoani Ruvuma ambako wanatekeleza mradi wa Tuwalinde ambao unahudumia watoto 423.

Naye Mwakilishi wa Balozi wa Marekani Jeremy Divis amesisitiza kuwa wapo tayari kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali yenye tija kwa jamii ukiwemo mradi wa tuwalinde ambao unatekelezwa pia mkoani Ruvuma.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...