Skip to main content

Ushirikishwaji Vijana Jengo la Halmashauri ya Mbinga ulivyomfurahisha RC Ibuge.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alipotembelea mradi wa ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga katika eneo la Kiamili.Mradi huo unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili hadi kukamilika.


Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Cosmas Nsenye akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge kuhusu vijana walivyoshirikishwa kwenye mradi huo kufyatua matofali ambayo yanatumika kutekeleza mradi huo.


Kikundi cha vijana wa Kigonsera ambacho kimeshirikishwa kwenye mradi wa jengo hilo kwa kufanyakazi ya ufyatuaji matofali ya kutekeleza mradi huo.


Msingi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Mbinga ambapo hadi sasa serikali imetoa shilingi bilioni moja kutekeleza mradi huo kupitia Mkandarasi SUMA JKT.


Na.Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mbinga kuwashirikisha vijana katika mradi wa ujenzi ofisi za Halmashauri hiyo unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili.

RC Ibuge ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea mradi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo unaotekelezwa katika eneo la Kiamili Kata ya Mkako wilayani Mbinga.

RC Ibuge ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo unaojengwa na SUMA JKT,ambapo amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji,Juma Mnwele.

Brigedia Jenerali Ibuge ameridhishwa na jitihada zinazofanywa kuwezesha jamii kupitia vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ikiwemo kikundi cha vijana cha Chipukizi ambacho kinajishughulisha na ufyatuaji wa tofali zinazotumika kwenye ujenzi wa jengo hilo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Juma Mnwele akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo,amesema hadi sasa zimeletwa shilingi bilioni moja na zaidi ya shilingi milioni 400 hadi sasa zimetumika kwa ajili ya hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi.

“Tumemkabidhi mradi SUMA JKT kuanzia Juni 2 mwaka huu,kwa kuanzia tumemlipa shilingi milioni 78,tunaridhika na utekelezaji wa mradi huu,vijana wameshirikishwa kikamilifu katika mradi huu’’,alisema Mnwele.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Mbinga amesema Kikundi cha Chipukizi kilichopo Kata ya Kigonsera mwaka huu 2021 kimenufaika kwa kupatiwa mkopo wa shilingi Milioni 22.

Amesema kikundi hicho ambacho kinashiriki kwenye mradi huo,ni miongoni kwa vikundi vingine zaidi ya 20 ambavyo vimewezeshwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 330 ikiwa ni asilimia 10 ya fedha za mapato ya ndani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa mwaka wa fedha 2020/2021hadi 2021/2022.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...