Shamba la Mfano likiwa na Mazao mbalimbali ikiwemo Mpunga wa Nchi kavu,Mahindi,Zao la strawberry, Bamia, Alizeti, Ufuta na mazao mengine ya Bustani kama Mchicha,chainizi,spinachi n.k. PICHA NA Swaum Katambo Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Laurent Munyu akifafanua jambo. Na Swaum Katambo, Mpanda-Katavi Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda inatarajia kutenga bajeti kwa ajili ya kuanzisha mashamba ya mfano ya kilimo cha kisasa ambayo yatasaidia kutoa Elimu kwa jamii juu ya namna bora ya kufanya kilimo cha kisasa hasa maeneo yaliyopo mjini. Akizungumza leo Mei 21,2020 katika hitimisho la hatua ya utoaji wa Elimu ya Kilimo kwa wakulima wa Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla,Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Laurent Munyu amesema pamoja na kuishi maeneo ya Mjini,Wananchi wanaweza kuandaa Mashamba na kulima Kilimo chenye tija. Munyu ameongeza kuwa wanachokifanya wanajar...