Skip to main content

JANE GOODALL YAWAJENGEA UWEZO WA ELIMU YA KUJITEGEMEA WANAFUNZI WILAYANI TANGANYIKA.


Mratibu wa Jane Goodall's Roots & Shoots Erasto Njavike akifafanua jamno.


Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Mhando akiwakabidhi Wanafunzi Mche wa Nanasi.


Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika akisisitiza jambo.


Na Swaum Katambo,Tanganyika-Katavi

Taasisi ya Jane Goodall kupitia Mradi wa Roots & Shoots imetoa Mizinga ya Nyuki 135 na Mbegu za Matunda Tani 1 pamoja na Miche ya Matunda ya Nanasi,Papai,Machungwa na Limao kwenye Shule za Msingi na Sekondari zilizopo Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi.

Akizungumza mara baada ya kutoa Mizinga,Mbegu pamoja na Miche hiyo Mratibu wa Jane Goodall's Roots & Shoots Erasto Njavike kupitia mradi wa Roots & Shoots amesema,walipoadhimisha miaka 60 ya utafiti wa Jane Goodall Mwaka Jana 2020,Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando alitamani kuona kila Shule iliyopo Wilayani humo inakuwa na Miradi hivyo mradi huo umetimiza kilio cha DC Mhando.

Njavike Ameongeza kuwa wanaamini Vijana wataisimamia vizuri Miradi hiyo ya ufugaji wa Nyuki pamoja na Matunda kisasa na kisayansi na kutumia fursa hiyo kumuomba OCD Wilaya ya Tanganyika kuwashughulikia Wezi wa Mizinga ya Nyuki endapo watajitokeza.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Makazi ya Mishamo Joseph Hosea amewapongeza Taasisi ya Jane Goodall kwa kuona umuhimu wa kuwajenga Vijana ngazi ya Shule za Msingi na Sekondari kuwa watunzaji wazuri wa mazingira huku akiwaomba kutoishia hapo na badala yake wazifikie Shule Mbili zilizosalia za Ifumbula na Isumbwe zilizopo katika Kata ya Mishamo.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando aliye kuwa Mgeni rasmi katika Hafla hiyo amesema Mradi huo utakwenda kuhuwisha maono ya hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere huku akiwapongeza Taasisi ya Jane Goodall kwa kufanyia kazi maono ya kuwajengea maarifa Watoto jinsi ya utunzaji wa mazingira na kusema kuwa wanawatengezea mfumo mzuri wa kuishi wafikapo ukubwani.

"Watoto ni Mabalozi wazuri kwani wakiwa watunza mazingira watawahamsisha wazazi,ndugu jamaa na marafiki pia kutunza Mazingira na hata ukubwani wataendelea kuwa watunza Mazingira kwa kuwa wana Msingi mzuri".Alisema DC Mhando.

Kadhalika DC Mhando ameongeza kuwa anatamani kati ya Miradi yote ya Jane Goodall basi Mradi huo wa Roots & Shoots upewe nguvu zaidi huku akiwataka Taasisi za Misitu kutenga kitengo cha Nyuki ili kuongeza Mizinga ya Nyuki katika Shule hizo kwani kufanya hivyo pia kutatengeneza Uchumi kwa Taasisi hizo.

Mbali na hivyo,Mhando amesikitishwa na taarifa aliyoipokea kuwa Mizinga hiyo ya Nyuki imetokea Mkoani Tabora huku akitamani angepewa taarifa ya kuwa Mizinga hiyo ya Nyuki imetokea Mkoani Katavi hasa Wilaya ya Tanganyika.

"Nataka tubadilike tuwe na mapinduzi ya kifikra,Mratibu amenipa taarifa nzuri sana..,Tumepokea Mizinga 135 ya kisasa kutoka Tabora.Kwanini Tabora? Kwanini isiwe Katavi? Kwanini isiwe Tanganyika? ndio swali langu la Msingi hapa".Alihoji DC Mhando.

Amesema kuwa Mkoa wa Katavi una Miti,Watu,Wataalamu wa nyuki pamoja na Viwanda hivyo ilipaswa Mizinga hiyo kutokea Mkoani Katavi hasa Wilaya ya Tanganyika na kusema kuwa jambo hilo ni udhaifu kwa kitengo cha Nyuki,Mratibu wa Nyuki na Wataalamu wa TFS kwani wamesomea vitu hivyo.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...