Baadhi ya Wananchi wakifatilia Mkutano wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Mhando,akiongea jambo mbele ya Wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Shukura.
Na Zainab Mtima,Tanganyika-Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani, Katavi Saleh Mhando
ameagiza watendaji wote wa vijiji katika halmashauri ya Wilaya ya
Tanganyika wanaoomba uhamisho,wasipewe
uhamisho wowote na badala yake warudi
katika vituo vyao vya kazi na kufanyiwa uchunguzi kama kuna deni lolote la
kijiji analodaiwa.
Mhando ametoa agizo hilo alipokutana na Uongozi
wa Kijiji cha Shukura ambapo Viongozi hao wamedai kuwepo na changamoto ya
uhamishwaji wa ghafla kwa Watendaji wa Vijiji jambo linalowaachia madeni yasiyo
ya lazima,kufuatia Watendaji hao kuondoka na michango ya Wananchi kwa ajili ya
maendeleo ya Kijiji.
Katika hatua nyingine Mhando ametoa Siku Saba kwa Uongozi wa Kijiji hicho kuhakikisha wanamaliza mgogoro wa eneo la ujenzi wa Shule ya Msingi Shukura na kuanza Ujenzi
wa Shule hiyo mara moja.
Hata hivyo Mhando
amewataka Serikali ya Kijiji cha Shukura pamoja na Watendaji wake,kufanya harambee ya kuilipa mifuko 50 ya saruji
iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa ajili ya ujenzi wa Shule hiyo
ambayo imeharibika.
Kijiji cha Shukura kilianzishwa Mwaka 2014 na ni Kijiji pekee katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ambacho hakina Taasisi
yoyote ya Serikali ikiwemo Shule wala Zahanati.
MWISHO.
Comments
Post a Comment