Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani.
Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda.
Na Mwandishi Wetu,Site Tv
Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa.
Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa.
Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya.
"Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwanda cha nguo kinaitwa Mpatex....kwa hiyo tunajenga hiki Kiwanda cha Mpatex na tumeandikiwa barua tumeambiwa tumepewa Milioni 360,kwa hiyo ni kufatilia tu kule tupate hicho Kiwanda cha Nguo na eneo limeshatengwa na Manispaa"-RC wa Mbeya Juma Homera,akimkabidhi Ofisi Mkuu mpya wa Mkoa wa Katavi
Nae Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Mrindoko amemshukuru Homera kwa kazi aliyoifanya katika Mkoa wa Katavi na kueleza kuyaendeleza yote mazuri aliyoyaacha ikiwemo kuibua mapya kwa maslahi ya Wananchi wa Katavi.
Aidha,amewaomba Viongozi kumpa ushirikiano kama walivyofanya kwa mtangulizi wake.
"Naomba ushirikiano Wenu kwa sababu peke yangu siwezi kuyafanya hayo,kama mlivyompa ushirikiano mwenzangu Juma,basi na Mimi mnipe ushirikiano"-RC Katavi.
RC Mrindoko amesema moja ya kipaumbele chake ni ukusanyaji mapato,usalama wa Mkoa ikiwemo utatuzi wa kero za Wananchi mapema kwa kuwa kutofanya hivyo kunaweza kupelekea Wananchi kujichukulia Sheria Mkononi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani amemtakia kila la kheri Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera katika majukumu yake na amemshukuru kwa namna alivyosukuma maendeleo katika Mkoa wa Katavi.
"Umefanya kazi kubwa kama alivyosema MNEC,umeukimbiza kimbiza!!! Umeukimbiza Mkoa!!? Nikupe sana hongera kwa hilo,na nikukaribishe tena"-Beda Katani, Mwenyekiti CCM Katavi.
Comments
Post a Comment