Raia wa Burundi waliokamatwa.
Na Jastin Cosmas,Kakonko-Kigoma.
Raia wa Burundi ambao ni Wafugaji,wamevamia ardhi ya Tanzania Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma kwa kuweka Mifugo ya Ng’ombe kama sehemu ya kuchunga kitendo ambacho kimeleta sintofahamu kwa Wananchi wa Kata ya Gwanumpu.
Sintofahamu hiyo imeibuka wakati Wananchi walipohoji katika mkutano wa hadhara ulio fanyika katika Kijiji cha Rusenga Kata ya Gwanumpu Wilayani Kakonko,ambapo wamelaani kitendo cha Mashamba yao kuvamiwa na Wafugaji kutoka Nchi ya Burundi huku mazao yao yakiharibiwa na Ng’ombe.
Wananchi hao wamesema kuwa,Mwnyekiti wa Kijiji cha Rusenga Evarist Ndumiwe alitoa ardhi kwa Wafugaji wa Burundi bila kushirikisha Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji hicho cha Rusenga.ambapo Wajumbe wa Kijiji hicho wamesema hawana imani na Mwenyekiti huyo.
Nae mwenyekiti wa Kijiji hicho Evarist Ndumiwe ametupilia mbali lawama hizo, akisema kuwa ameingia kwenye uongozi Ng’ombe hao wakiwepo hivyo haja ruhusu Ng’ombe hao kuingia Tanzania.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Gwanumpu Toyi Butono amesema kuwa Ng'ombe hao waondolewe,sheria na taraibu zifatwe na ardhi irudishwe kwa Wananchi.
Ntarabe Mvulugu,ni miongoni mwa Wananchi ambao Mashamba yao yamevamiwa ambapo amesema kuwa tayari Mazao yake yameharibiwa na Ng’ombe,na hana sehemu nyingine yakulima kwani alikuwa anategemea sehemu hiyo kwa shughuli ya Kilimo.
Site Blog imemtafuta Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama ambae ni Mkuu wa Wilaya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala ambapo amesema kuwa hajapata taarifa kuhusu kuwepo kwa Ng’ombe hao hivyo suala hili atalifuatilia kwa kina.
Msikilize hapa chini Diwani wa Kata ya Gwanumpu Toyi Butono.
Comments
Post a Comment