Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Hoza Mrindoko katika Kikao na Watumishi wa Umma Mkoani Katavi cha kusalimiana na kufahamiana leo Mei 24,2021.
Katibu Tawala Mkoa wa Katavi,Abdallah Mohammed Malela.
Baadhi ya Watumishi wa Umma wakifatilia Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa Kikao cha kusalimiana na kufahamiana katika ukumbi wa Mpanda Manispaa.
Na Mwandishi Wetu,Site Tv
Mpanda-Katavi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ndg. Abdallah Malela amemweleza Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Hoza Mrindoko kuwa Watumishi wa Mkoa wa Katavi wanafanya kazi kwa kujituma bila kujali Siku za Kazi na hawana changamoto zozote isipokuwa Mkoa unatatizo kubwa la Lishe na Matundu bora ya Vyoo.
Ameyasema hayo wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Bi.Mwanamvua Hoza Mrindoko katika kikao na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Katavi,Kikao cha kusalimiana na kufahamiana kilichofanyika katika Ukumbi wa Mpanda Manispaa leo Mei 24,2021.
Kwa upande wake RC Mrindoko ametumia nafasi hiyo kuwashukuru Watumishi wenzake kwa mapokezi na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini huku akisema atahakikisha anatimiza yale yote yanayotarajiwa na Rais kwa Wanakatavi kutoka kwake na kuwataka Watumishi kuendelea kujituma kwa kufanya kazi vizuri kwa manufaa ya Wananchi.
"Nimeona cha Kwanza kabisa nikutane na nyie,kwa sababu naamini kwamba hii ndiyo timu ya ushindi,lakini kwa Miaka hii takribani 9 sidhani kuna jipya kujiita Mkoa mpya,kwa hiyo sioni sababu ya kujiita Mkoa mpya kwa sababu tayari zipo hatua kubwa ambazo tumeshapiga Sisi kwama Mkoa wa Katavi"-RC Katavi,Mwanamvua Mrindoko.
RC Mwanamvua amesema kila nafasi katika Uongozi inaumuhimu wake katika kusimamia miradi kwa ukamilifu hivyo ni wito wake kuona mipango yote inatekelezwa kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwemo kuisoma na kujua nini kinatakiwa kufanyika katika kila Sekta.
Aidha,amesema ni jukumu la kila Mmoja kuhakikisha usalama wa Mkoa,na amewasihii Watumishi kutoa taarifa pale wanapoona hali ya uvunjifu wa Amani ili hatua zichukuliwe kabla ya madhara kutokea huku akiwataka kuzitunza Mali za Umma kama wanavyotunza Mali zao.
Kadhalika amewaomba Watumishi wote Kutenda haki katika kuwahudumia Wananchi ikiwa ni pamoja na kuepuka ubaguzi kwa Maslahi yao Binafsi na badala yake kuwahudumia Wananchi kwa haraka na kutatua changamoto zao huku akiikemea sentensi ya "rudi kesho" na kusema kuwa asingependa kuisikia.
Kwa upande wao baadhi ya Watumishi wa Umma wamemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa watafanya kazi kwa ushirikiano.
Comments
Post a Comment