Pichani ni Washiriki wa kikao kazi cha kujenga uelewa wa Wadau juu ya awamu ya 3 ya Kipindi cha Pili cha Shughuli za TASAF,kikao kilicho wakutanisha Madiwani,Wataala,Wana Habari na Wawezeshaji. Picha na Elias Mlugala.
Judith Woiso,Afisa Ufuatiliaji-TASAF,akitoa elimu kwa washiriki wa Semina.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhi3NRCtRSzYFiFO202O8ndZ6HGF9h1M3Ijl33i_En9PrEqt6Ky22x0ROUJoqrqTSGHhnsqTJEOJlpcQEgGmOJ0yS_5PP5DKfqV7OeOPeFUqkPwdLIELPMIwWUEpvazJEBKBvm5Rh36e-Y/w640-h360/vlcsnap-2021-05-26-08h47m24s957.png)
Zacharia Ngoma,Mwakilishi wa Mkurungenzi Mtendaji wa TASAF akitoa neno.
Na Mwandishi Wetu,Site Tv.
Madiwani wa Halimashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wametakiwa kutoingilia mfumo wa usajili wa Wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili kuondoa uingizaji wa Wanaufaika wasio na sifa.
Wito huo umetolewa na Zacharia Ngoma,Mwakilishi wa Mkurungenzi Mtendaji wa TASAF katika kikao kazi cha Madiwani,Timu ya Wataalam kutoka TASAF Makao Makuu,Wana Habari na Wawezeshaji cha kujenga uelewa wa Wadau juu ya Sehemu ya Pili ya awamu ya 3 ya Shughuli za TASAF,kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mtakatifu Mathias,uliopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.
"Vipo vigezo vya kuziingiza Kaya masikini,vipo vigezo vya kuzitambua kaya masikini,pamoja na vigezo vyote lakini Wananchi wenyewe wataweka vya kwao wenyewe kuitambua ipi kaya ambayo ina hali duni,kwa hiyo tuwaachieni Wananchi wafanye kazi wao,Sisi Waheshimiwa tukiliingilia zoezi mwisho wa siku tutakuja kuambiwa tumeingiza Kaya zisizo na sifa"-Amesema Zacharia Ngoma.
Awali akifungua Mafunzo hayo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Zacharia Ngoma amesema Kipindi cha Pili cha awamu ya Tatu ya TASAF kilizinduliwa Februari 17,2020 Jijini Dar Es Salaam ambapo Serikali iliagiza itolewe Elimu ya kutosha kuhusu mpango huo wa TASAF na namna ambavyo walengwa wanapatikana ili kuondoa malalamiko kwenye Jamii.
Pia amesema muundo wa kipindi cha Pili cha awamu ya Tatu ya TASAF umezingatia changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa kipindi cha Kwanza hivyo awamu hii wamekuja na maboresho zaidi kwa kuhakikisha elimu kwa walengwa inatolewa kila wakati.
Ngoma ameongeza kuwa,Wasimamizi na Viongozi wanalojukumu la kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji katika ngazi zote kuanzia Mkoa,Halmashauri,Kata mpaka kwenye ngazi ya Jamii kwa kuhakikisha Watumishi wanafuatilia shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii hasa zile zinazo husu ustawi wa Walengwa ili zilete tija.
Akifunga Mafunzo hayo Kaimu katibu Tawala Wilaya ya Mpanda Ipyana Kakuyu ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza dhamira ya Nchi ya kupunguza umasikini na kuboresha upatikanaji wa huduma za Jamii ambazo ni pamoja na Elimu,Afya na Maji kwa kushirikisha Jamii na kukuza dhana ya kujitegemea.
Kwa upande wao baadhi ya Madiwani Rafael Kalinga Diwani wa Kata ya Machimboni na Gerimana Mwanandota Diwani Viti maalum Halimashauri ya Nsimbo kutoka Kata ya Mtapenda wamesema wameyafurahia mafunzo kwa kuwa yamelenga kwenda kuondoa changamoto zilizojitokeza katika mfumo uliopita.
Licha ya kufurahia mafunzo hayo,Bi.Mwanandota ameishauri Serikali kuangalia upya utaratibu uliowekwa wa ili mnufaika apate Pesa lazima awe na Simu au akaunti ya Benki kwa kile alichodai siyo wote wana uwezo wa kumiliki Simu au kufungua akaunti.
Halimashauri ya Nsimbo ina Vijiji 54 ambapo kati ya hivyo ni Vijiji 13 pekee vyenye Mradi wa TASAF,ambapo imeelezwa kila Mwaka wanaufaika Elfu 8 wanatoka kwenye mfumo kutokana na wengine kufariki,kuhamia sehemu nyingine na wengine kupata mafaniko kupitia mradi huo.
Awamu ya Tatu ya Kipindi cha Pili cha Shughuli za TASAF kina tarajia kufikia Kaya Milioni Moja na Laki Nne na Nusu,zenye Jumla ya Watu zaidi ya Milioni 7 kote Nchini.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhDRcULJBCWUmWQ1AWZr6Khr-7SKkpwOXQntG3cPOrYpDTc2m4YPnhcbCa-9Yuozi88X12RJEC5zO7GaI_WFtCJMHQ0d4fhM4QA61A5ffpSuaj-Urka4E6i0ojxZIdEOHyE22sdNAGrQTg/w640-h360/vlcsnap-2021-05-26-08h47m47s962.png)
Rafael Kalinga Diwani wa Kata ya Machimboni,akizungumza na Site Tv kuhusu Elimu waliyopewa na namna atakavyokwenda kuyatekeleza katika eneo lake.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh6cw69LBtHXRIOgPOPLRGSvSjvshhgV19kd-webH16n6K57-O5YO5OtdA3-x9SWE5WWHnr7H2LvlMr8ZVOHdYAPJGhe2X7kGg2crc8Kqk0htQ0-Q06TfJHDaGXp4yztGGt4xF3l1SW6Bc/w640-h360/vlcsnap-2021-05-26-08h47m57s208.png)
Gerimana Mwanandota,Diwani Viti maalum Halimashauri ya Nsimbo kutoka Kata ya Mtapenda.
Comments
Post a Comment