Na Zainab Mtima,Tanganyika-Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi,Saleh Mhando amewasimamisha
kazi Mwenyekiti wa Kijiji cha Shukura Peter Colomery na Mtendaji wa Kijiji
hicho Mesamo Megama ili kupisha uchuguzi kufuatia tuhuma za ubadhilifi wa Fedha
zilizochangwa na Wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Shukura.
Mhando ametoa maagizo hayo katika mkutano wa hadhara na wakazi
wa Kijiji hicho,ambapo awali walitoa kero zao mbele ya Mkuu wa Wilaya huyo na
kuzipatia ufumbuzi na kuongeza kuwa Watumishi hao watachunguzwa na taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilayani Tanganyika. .
Katika mkutano huo pia Mhando ameagiza Uongozi wa Kijiji hicho kuhakikisha ujenzi wa Shule ya Msingi Shukura kuanza kujengwa
kuanzia June Mosi Mwaka huu.
Hata hivyo ametoa tahadhali kwa Wananchi waishio
pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,kuepuka kujenga makazi ya kudumu maeneo ya
mwambao wa ziwa .
Aidha amewataka Wenyeviti wa Vijiji vyote katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kusoma mapato na matumizi kwa Wananchi kila
baada ya Miezi Mitatu.
MWISHO.
Comments
Post a Comment