Skip to main content

Wasimamishwa Kazi baada ya kulipana Posho.

Waziri Mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa.


Na Mwandishi Wetu

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu,mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha  za umma zinazowakabili.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28,2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango,katibu mkuu,manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana,Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru),Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.

Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31,2021 kupitia vocha 30 ya TSh. Milioni 251 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.

Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa TSh. Milioni 198.8 kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8,2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa  TSh. Milioni 44.5 za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni  kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Pia Aprili 30,2021 zililipwa TSh. Milioni 43.9 kwa ajili ya kuandaa  mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa TSh. Milioni 14.4 kwa ajili ya siku ya wanawake.

Inaeleza kuwa fedha nyingine TSh. Milioni 43 zililipwa siku hiyo na kufanya  jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa TSh. Milioni 101.8.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni  na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni  zikiwa ni malipo ya kazi maalum.

"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,”-amesema Majaliwa.

Inabainisha kuwa Mei 3,2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa  watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo  ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni  kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni  zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa  wapi? Mnazidi kutupunguzia imani,  na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha  kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,”-amesisitiza Majaliwa.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.

CHANZO:Mwananchi

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja