Shamba la Mfano likiwa na Mazao mbalimbali ikiwemo Mpunga wa Nchi kavu,Mahindi,Zao la strawberry, Bamia, Alizeti, Ufuta na mazao mengine ya Bustani kama Mchicha,chainizi,spinachi n.k. PICHA NA Swaum Katambo
Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Laurent Munyu akifafanua jambo.
Na Swaum Katambo,Mpanda-Katavi
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda inatarajia kutenga bajeti kwa ajili ya kuanzisha mashamba ya mfano ya kilimo cha kisasa ambayo yatasaidia kutoa Elimu kwa jamii juu ya namna bora ya kufanya kilimo cha kisasa hasa maeneo yaliyopo mjini.
Akizungumza leo Mei 21,2020 katika hitimisho la hatua ya utoaji wa Elimu ya Kilimo kwa wakulima wa Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla,Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Laurent Munyu amesema pamoja na kuishi maeneo ya Mjini,Wananchi wanaweza kuandaa Mashamba na kulima Kilimo chenye tija.
Munyu ameongeza kuwa wanachokifanya wanajaribu kuonesha wadau wa Kilimo namna bora za uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali kama Mpunga wa Nchi kavu,Mahindi,Zao la strawberry, Bamia, Alizeti, Ufuta na mazao mengine ya Bustani kama Mchicha,chainizi,spinachi n.k
"Kitu tunachokifanya leo ni moja ya majukumu mazito sana ambayo Idara ya Kilimo inapaswa kufanya,sisi wataalamu wa Kilimo tunaamini jambo moja kwamba kuona ni kuamini..,tunachokifanya ni kufanya sisi kwa mfano mpaka tunafikia matokeo,yale matokeo sasa ndio tunakuja kumuonesha Mkulima na kumuelekeza njia ya kuyafikia yale matokeo" Alisema Munyu.
Kwa upande wao baadhi ya wadau wa Kilimo walionufaika na Elimu ya Kilimo hicho cha kisasa wameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa kuandaa mafunzo hayo ambapo wamesema walizoea kulima Kilimo cha maeneo ya bondeni ili kufuata maji hivyo Elimu hiyo imewapa mwanga kuwa wanaweza kulima hata maeneo ya nchi kavu yaliyopo mjini na kupata mazao yenye tija.
Baadhi ya Wadau wakieleza namna watakavyoitumia Elimu waliyoipata kujikwamua katika Kilimo.
Comments
Post a Comment