![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRkFwjC0JYuY8o9NjDgXzJkqJPZYjYzmSQYu-ffD3wt1OD-u21c9voHllQ8xr-TuMGfNZjHKeHP1MvwkS9SC9mVlgb4niWClIdS6AcAhMFXVh7lvATE-snPdNY6_oGb__zA_eBonckHOw/w640-h360/IMG-20210527-WA0026.jpg)
Mkuu wa Wilaya ya Mlele,Rachel Kasanda akitoa maelekezo ya jambo fulani.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgcFAEQQVfbErB2fomfkkLsihYZbwk3oVaAchi87mVHdpVir9TUoUsJiqHjXPlj5SMNspoNEkoRrAtJ5bQMsQgF7ZrVUJDqSvEjsLV0OFt7EyIuabn8ApKRrRtIEGammUuf7LMjceoBSow/w640-h426/IMG-20210528-WA0004.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGMoW8L7-S86lznC3_9S6r9gYloXHT-68rCDsCLnVVYFGowAa045PqCf_WL9W7YuzsgONjoL8jsK9Pr2EM5resRbd7Vl8HRuTcPwiboRXg54StzTdQhaeSEwUWRBjUygBJUVb93W8LjMk/w640-h426/IMG-20210527-WA0032.jpg)
Mradi wa ujenzi wa Wodi 3 ikiwemo Wodi ya Watoto,Wanawake na Wanaume.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEillJbdxXMkMc_SB5aS4VWorIlqNs0cf7rXkrIacS9BcNJRSC3aqpKZeX6Yz-_fRfaKkpVS0KHmtxygHsXs21ou6gNOjcjqc1NcftT3S21WYw9wEFICGoKehqwIid5DnQFDYf9tUs4MHlM/w640-h360/IMG-20210527-WA0030.jpg)
Zahanati ya Mirumba inayojengwa.
Nyumba ya Mkurugenzi inayojengwa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgFgSgvrfNg8yiwlndtqXfQzg5qbjigjydeKIN7jd9023dvO-4BaY2CGC3aB5yV261qP4KruAJO4WwPymdIwAJUsOrzN4-Vu0Sn_S3qQUr-2U5BmmltAVX4sYdumojwbhLMisobGBIt7kY/w640-h426/IMG-20210528-WA0001.jpg)
Nyumba za Wakuu wa Idara. Picha na Swaum Katambo.
Na Swaum Katambo,Mpimbwe-Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda Jana Mei 27,2021 amefanya ziara ya kutembelea Miradi ya Ujenzi wa Zahanati ya Mirumba iliyopo Kata ya Kibaoni,Ujenzi wa Wodi Tatu ya Watoto,Wanawake na Wanaume katika Hospitali ya Halmashauri na Ujenzi wa Nyumba Saba za Wakuu wa Idara na Vitengo na Uzio.
Katika Ziara yake ya kukagua Ujenzi wa Zahanati ya Mirumba iliyogharimu kiasi cha Tsh. 46,953,000/- ambapo ndani yake kiasi cha Tsh.26,953,000/- zilitokana na michango ya nguvu za Wananchi ambapo DC Rachel Kasanda ametumia fursa hiyo kuwapongeza Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe kwa ushiriano wanao utoa kwa Serikali katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali.
"Huu ni mfano wa kuigwa hata katika Halmashauri nyingine watu wanaweza wakaiga,tumekuwa tunaenda mbali sana kwa sababu ya ushirikiano tunaoupata kwa Wananchi,hata kama mradi tunatumia mapato yetu ya ndani lakini ushiriano unakuwa mkubwa sana wa Wananchi kujitoa kufanya kazi ambazo zimekuwa zikisaidia kutekeleza mradi mmoja lakini pia na kuongeza jengo lingine zaidi kwa sababu ya ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi"-Alisema DC Kasanda.
Hata hivyo DC Kasanda ameshauri usimamizi wa Ujenzi wa Choo katika Zahati ya Mirumba ukamilike haraka kwani Wananchi wanaendelea kupata huduma katika jengo la Zamani hivyo ni vyema angalau wapate mazingira yaliyo rafiki kwa haraka zaidi kwa ajili ya kutolea huduma huku akitoa maelekezo ya kuweka Marumaru kwenye Vyoo hivyo ili kuepuka mipasuko itakayoweza kutokea pindi yatokeapo matukio ya Tetemeko la ardhi.
"Majengo mengi ambayo tumekuwa tukijenga katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe yanachanika,nyufa zinaanza kuonekana kwenye sakafu chini kwa sababu ya matetemeko ambayo mara nyingi yamekuwa yakijitokeza ya dharura ambayo sisi hatuwezi kuyazuia katika hali ya kawaida"-Alisema DC Kasanda.
Katika taarifa ya awali iliyosomwa na Mtendaji wa Kijiji cha Mirumba Maria Chitimbwa alisema kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kiasi cha Tsh.75,000,000/- kimetengwa kupitia bajeti ya ruzuku kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ukamilishaji wa Zahanati hiyo na mpaka sasa kiasi cha Tsh.50,000,000/- kimepokelewa kutoka Serikali kuu kwa ajili ya Ukamilishaji wa Zahanati ya Mirumba.
Kadhalika,Mradi huo umesaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya kwa Wananchi wa Kijiji cha Mirumba na Vitongoji vyake katika utoaji wa huduma za kinaMama wajawazito,Wagonjwa pamoja na Watoto ambao hapo awali iliwalazimu kutembea umbali wa Kilometa 6 kwenda kupata huduma katika Zahanati ya Kibaoni.
Katika hatua nyingine DC Kasanda ametembelea mradi wa Ujenzi wa Wodi Tatu (Watoto,Wanawake na Wanaume) katika Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe unaotekelezwa kwa mfumo wa Force Account ambao ulikadiriwa kutumia kiasi cha Tsh. Mil.500,ambapo hadi sasa ujenzi wa majengo hayo uko hatua ya Boma na umeshagharimu kiasi cha Tsh. 331,725,230.39.
Mradi huo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa Wananchi wapatao 147,685 waliopo katika H/W ya Mpimbwe ikiwa ni pamoja na kuhudumia Wanawake,Wanaume na Watoto waliokuwa wanapata matatizo makubwa ya kiafya na kutembea umbali wa Kimometa 125 kwenda Hospitali ya Mkoa wa Katavi kufuata huduma.
Mbali na hayo DC Kasanda pia alipata fursa ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 7 za Wakuu wa Idara na Vitengo na Uzio ambapo Halmashauri inatekeleza mradi huo kwa kutumia mfumo wa Force Account kwa kiasi cha Tsh, Mil.500 kilichotengwa katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/2021.
Mradi huo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa Watumishi ambao ni Wakuu wa Idara 7,jambo litakalo rahisisha Watumishi kuwa karibu na eneo la kazi na kuweza kuwa na ari na ufanisi katika utendaji wa kazi kila siku na mradi huo unafanya kuwa na jumla ya Nyumba 19 ambazo zilijengwa hapo awali ikiwemo nyumba moja ya Mkurugenzi Mtendaji.
Akihitimisha kukagua Miradi,DC Kasanda ametoa Mwezi Mmoja kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe kufikia Juni 28,2021 ahakikishe anasimamia marekebisho ya Milango ya Hospitali ya Halamshauri,iliyopo Kata ya Usevya ambayo Milango hiyo imejengwa chini ya kiwango ukilinganisha na hadhi ya Hospitali.
Agizo hilo linakuja mara baada ya DC Kasanda kutoridhishwa na ubora wa Milango hiyo wakati akikagua Mradi wa Ujenzi wa Wodi Tatu za Watoto,Wanawake na Wanaume,katika Hospitali ya Halmashauri ambapo Mwaka jana wakati akikagua mradi huo hakuridhishwa na milango hiyo na kulazimika kuitolea maagizo ya kubadilishwa na baada ya kubadilishwa mara ya pili pia hakuridhishwa na kiwango cha milango hiyo kulingana na hadhi ya Hospitali.
"Hii milango ibadirishwe,mwezi mmoja tuu nataka ibadilishwe,nimesema hata kwenye makabidhiano ikitokea sipo hapa hii kazi iishe,yaani hilo mumwambie Mkurugenzi am serious mwezi mmoja kazi ibadilike kabisa,iwe katika ufasaha ambao nataka"-DC Mlele,Rachel Kasanda.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda kufanya ziara ya kutembelea Miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe tangu mara ya mwisho alipopata ajali mnamo Octoba 2,2020 wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi katika Halmashauri hiyo na baada ya ajali,alikuwa akipatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili.
MWISHO.
Comments
Post a Comment