Na Mwandishi wetu,Site Tv Nanenane-Mbeya #NEWS Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera ameridhishwa na bidhaa za Wafanyabiashara kutoka Mkoani Katavi,baada ya kutembelea mabanda yao katika maonyesho ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayoendelea viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya. Homera akiwa ameambatana na Viongozi wengine akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu Abdalah Malela,Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda,Mh. Salehe Mhando wa Tanganyika na Jamilla Kimaro wa Mpanda baada ya kutembelea baadhi ya Mabanda amesema. "Nimefarijika na namna maandalizi yalivyofanyika,kiukweli Mkoa wa Katavi wamejipanga vizuri,nimeona kwenye mabanda yao yanaridhisha,yanaendana na kauli mbiu ya Mheshimu Rais wetu Tanzania ya Viwanda,unaweza kuona wametengeneza Wine nzuri, wametengeneza unga mzuri, wametengeneza asali vizuri,na wana Viwanda vya asali kwa mfano ukienda kule Bulamata na maeneo mengine" -Alisema RC Homera, alipotembelea mabanda ya Nanenane. "Lakini Manispaa n...