Skip to main content

RUWASA Songea yatoa mafunzo na vyeti kwa jumuiya tisa za watumia maji




Katibu Tawala Wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro akigawa vyeti kwa wanajumuiya za maji wilaya ya Songea baaada ya kupata mafunzo kutoka RUWASA wa maji vijijini 

RUWASA wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imetoa mafunzo na kugawa vyeti kwa jumuiya tisa za watuamia maji katika Halmashauri za Madaba na Halmashauri ya Songea.

Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Songea Klub Mtaalam wa RUWASA Wilaya ya Songea Samweli Sanya amesema Ruwasa kwa kushirikiana na jumuiya hizo zilizoundwa watahakikisha wananchi wanapata huduma ya maji endelevu kwa usimamizi na uendeshaji na wananchi watachangia huduma hiyo.

Mgeni rasimi katika mafunzo hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro amesema lengo la RUWASA ni kutekeleza na kuiwezesha jamii kuwa na jumuiya ya maji imara na kuleta tija endelevu kwa wananchi vijijini.

Amesema Jumuiya waliopata mafunzo hayo wawe walimu na wasimamizi wazuri katika kutunza miundo mbinu iliyopo katika jumuiya za watumia maji ili wananchi wapate huduma bora na endelevu.

‘’Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuunda wakala wa maji safi na mazingira vijijini RUWASA inatusaidia kuleta huduma nzuri karibu na wananchi wa vijijini’’,alisema.



Jumuiya tisa za maji  katika wilaya ya Songea zikipewa mafunzo ya watumia maji kutoka  RUWASA yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Songea klub

Ndumbaro amesisistiza kuwa Jumuiya tisa zilizopata mafunzo hao zihakikishe wananchi wanapata huduma nzuri ya maji na watunze mazingira,Serikali imetoa fedha nyingi katika miradi mikubwa ya maji ambapo amewaasa wananchi kutunza vyanzo vya maji na kuacha kukata miti hovyo.

‘’Nitolee mfano mzuri katika milima ya Lihanji wilayani Songea kuna vyanzo vya maji na vyanzo vyake vinalisha maeneo makubwa katika tarafa ya Ruvuma Peramiho na Kilagano vinatumia kutoka milima ya Lihanji’’,alisisitiza.

Amesema licha ya mafunzo waliyopata kuna rasimu ambazo zimetolewa na kupitishwa Jumuiya zote ambazo ameagiza wakasimamie na kwamba miundombinu inapoharibika irekebishwe kwa kutumia michango wanayochangisha kwa wananchi.

RUWASA imeanzisha kupitia sheria namba tano iliyopitishwa na Bunge mwaka 2019 na kuanza kutumika Julai mosi 2019.

Imeandikwa na Anet Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja