Skip to main content

WAZIRI Mkuchika amwakilisha Rais Magufuli ufunguzi ofisi ya TAKUKURU Namtumbo

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu Gorge Mkuchika amemwakilisha Rais Magufuli katika ufunguzi wa jengo la ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Namtumbo lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 139.

Akizungumza kabla ya kufungua jengo hilo katika hafla iliyofanyika mjini Namtumbo Waziri Mkuchika amesema Rais Dkt.John Magufuli amemteua kufungua jengo hilo kwa niaba yake na kwamba Rais ameweka utaratibu wa kuyafungua majengo mapya ya TAKUKURU kwa nyakati tofauti na wasaidizi wake.

Ameagiza majengo mapya saba ya TAKUKURU ngazi ya wilaya yatumike vema katika mapambano dhidi ya rushwa pamoja na kuwafichua wala rushwa sanjari na kuacha kushiriki katika vitendo vya rushwa.

“Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Jemedari Rais wetu,imefanya kazi kubwa ya kuimarisha na kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini’’,alisisitiza Waziri Mkuchika.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt.Mstaafu Gorge Mkuchika akifungua ofisi ya TAKUKURU Namtumbo

Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika,ripoti ya Benki ya Dunia ya Septemba 26,2019,imeeleza kuwa Tanzania imeongoza kwa kupunguza umaskini miongoni mwa nchi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kulingana na Waziri Mkuchika,ripoti nyingine ya Benki ya Dunia inayoitwa Human Capital,The Real Wealth Of Nationals iliyotoka Julai 2019 ilionesha kuwa umasikini nchini Tanzania umepungua kutoka asilimia 34.4 hadi kufikia asilimia 26.8.

Waziri Mkuchika amesema ufanisi wa jitihada za serikali katika mapambano dhidi ya rushwa nchini katika mwaka 2018/2019 zimeendelea kuonesha pia kupitia taarifa za utafiti wa kupima hali ya rushwa duniani unaofanywa na wadau wa mapambano dhidi ya rushwa na utawala bora kama Taasisi ya Transparency International, MO Ibrahim na Afro Barometer.

“Taarifa za Taasisi hizo zote kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 zinaonesha kuwa Tanzania imeendelea kufanya vyema katika mapambano dhidi ya Rushwa’’,alisisitiza Mkuchika. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU aliyewakilishwa na Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa wa TAKUKURU Sabina Seja amesema jengo hilo ni moja kati ya majengo mapya saba ya TAKUKURU ngazi ya Wilaya yaliojengwa kwa wakati mmoja.

Ofisi mpya ya TAKUKURU wilaya ya Namtumbo iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 139

Seja amesema TAKUKURU katika Mkoa wa Ruvuma hadi kufikia Juni 2020 imefanikiwa kuchunguza ubadhirifu na kuokoa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 740.

‘Fedha hizo zimeweza kuokolewa kutokana na uchunguzi katika Benki ya wananchi wa Mbinga,vyama vya ushirika na kuwezesha baadhi ya watuhumiwa kurejesha fedha,vitendo hivyo vya ubadhirifu vilikuwa vinadumaza maendeleo ya ushirika nchini’’,alisema Seja.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza katika hafla hiyo amewaasa TAKUKURU kuendelea kuwang’ata wala rushwa na mafisadi wote bila kuwaonea na kuwapendelea ili kutomekeza rushwa nchini.

Mndeme amesema jengo hilo la TAKUKURU wilaya ya Namtumbo litaimarisha utendaji kazi wa watumishi wa TAKUKURU na kurahisisha watoa taarifa na mashahidi watakaoletwa katika opereshani mbalimbali za mapambano ya rushwa na kufanya kazi kwa uhuru na usiri zaidi.

Imeandikwa na Albano Midelo 

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Namtumbo

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja