Na Mwandishi Wetu.Katavi.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeziomba Halmashauri zote nchini kutumia fursa za kufungua anuani za makazi (Post Code) ili kuboresha maisha ya wananchi kupitia huduma za mawasiliano.
Kauli hiyo imetolewa hapo jana kwenye semina ya siku moja katika ukumbi wa Idara ya maji Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi na Mhadisi wa Mamlaka hiyo kanda za Nyanda za Juu Kusini,Charles Thomas alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani humo.
Mhandisi Charles aliziomba halmashauri kuwa kitendo cha kufunguliwa wa anuani za makazi kwenye halmashauri zitachochea ukuaji katika sekta ya mawailiano nchini ikiwa pamoja kutumia fursa za tehema hasa mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa maendeleo.
Akifafanua umuhimu wa anuani za makazi kwa Halmashauri Mhadisi huyo alibainisha kuwa zitaweza kusadia katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na kodi kwa wananchi kwani watakuwa na takwimu halisia za anuani za makazi ya watu wanapoishi au biashara zao wanapo fanyia hivyo kusaidia kuwafikia kwa haraka.
Vilevile kusaidia katika mazoezi mbalimbali ya kitaifa kama vile undikishwaji wananchi yaani sensa,kuongeza utalii,kufanya tafiti, pamoja na undikishwaji wa mali kama vile nyumba,biashara,wapiga kura.
"...mwaka 2002 kwenye zoezi la mwisho kufanyika la sensa kuna baadhi ya maeneo ilikuwa ni ngumu kufika kwa sababu ya kutokujua welekeo halisi wa makazi ya watu "Alisema Mhadisi Charles.
Pamoja na hayo Halmashauri zimeombwa kuomba mafunzo maalumu kutoka mamla ya mawasiliano nchini mafunzo ambayo yatawaongeza uwezo kwa maafisa wa Halmashauri katika kutekeleza zoezi zima la ufunguaji wa anuani za makazi.
Katika hatua nyingine Afsa masoko wa TCRA Nyanda za Juu kusini Elias Joseph aliweka wazi kuwa mamlaka hiyo wajibu wake ni kuweka mazingira sawa ya utendaji kazi ili kuimarisha ushindani wa haki na kukuza maendeleo ya kiuchumi.
Aidha alibainisha kuwa ni kulinda masirahi ya wateja kama vile watumiaji wa mitandao mbalimbali ya simu ikiwa pamoja na kusimamia rasilimali masafa na namba zinazotumika katika utoaji wa huduma za mawasiliano ya simu.
Joseph alisema kuwa kwa kuzigatia shughuri za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi katika kuimarisha tafiti zenye ubora wa huduma zinazodhibitiwa ,uwezo,na umahiri wa watumiaji.
Vilevile aliwapa tahadhari kubwa wananchi kuepuka kununua simu kiholela bali wazingatie kununua kwenye maduka ambayo yamesajili kwenye mamlaka hayo huku wakihakikisha wanadai list za malipo pindi wanaponunua simu zao.
Kwa upande wa kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika Gwamaka Owden wakifunga semina hiyo licha ya kuishukuru TCRA Nyanda za Juu kusini alisema kuwa zoezi la kuazisha anuani za makazi kwa wananchi watalitekeleza haraka iwezekanavyo ambapi litawasaidia katika upangaji mji.
Oweden aliiambia TCRA kuwa hawatasita kuchua hatua yoyote ikiwame ya kuomba mafunzo maalumu kutoka mamlaka hiy0 pindi itakapohitajika katika kuboresha ufanisi wa utengenezaji wa anuani za makazi.
Comments
Post a Comment