Na Swaum Katambo,Site News
Mpanda/Tanganyika,Katavi.
Mkandarasi anayejenga Tanki la Mradi wa Maji ya Ikolongo 2,Millennium Master Builders LTD amemuahidi Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuwa hadi ifikapo Septemba 15 mwaka huu Mradi huo utakuwa umekamilika
Ametoa ahadi hiyo leo Agosti 10 kwa njia ya Simu alipopigiwa na Naibu Waziri Aweso alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa tanki kubwa lililopo Mtaa wa Mapinduzi katika kata ya Ilembo Manispaa ya Mpanda ambapo ameeleza kuridhishwa na utendaji ikiwemo usimamizi wa miradi ya maji vijijini chini ya Wakala wa maji vijijini RUWASA.
Mradi wa Tanki la Maji Mapinduzi wenye ujazo wa Lita Milioni Moja unaosimamiwa na Mkandarasi wa Millennium Master Builders LTD
Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mpanda (MUWASA) Eng.Iddo Richard akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa miradi ya maji amesema mradi huo ukikamilika utazinufaisha zaidi ya Kaya 30,000 na utakuwa na uwezo wa kutoa kiasi cha lita zaidi milioni sita ambazo sawa na asilimia 60 ya mahitaji ya huduma ya maji katika Mji wa Manispaa ya Mpanda.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizindua Bomba la Maji la Mradi wa Majalila Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi.
Katika hatua nyingine ameitaka Mamlaka ya Nishati na Maji EWURA ijitathimini kutokana na kushindwa kuingilia kati suala la Mamlaka za maji nchini Tanzania kupanga bili za maji bila kumshirikisha mteja
Aidha Naibu Waziri Juma aweso akiwa wilayani Tanganyika amesema serikali imetoa Bilioni Tano kwaajili ya kukamilisha miradi ya maji vijijini chini ya Wakala wa maji RUWASA ikilenga kufikisha utoshelevu wa 85%.
Kufuatia changamoto zinazojitokeza katika ulipaji wa bili za maji Nchini,zikiwemo kupata bili kubwa pasipo matumizi halali Mh Aweso amezitaka Malaka za Maji Nchini kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya usomaji wa Mita kwa kushirikiana na watumiaji.
"Kutoshirikishwa Wananchi juu ya ulipaji wa Bili za Maji huwezi ukamletea mtu meseji,huwezi ukaenda kwa Mtu unasoma bili ya Maji kwenye Mita pasipo kumshirikisha mwenyewe,hilo jambo tumelitolea maagizo,pia unapomshirikisha lazima akasaini kwamba hapa leo tumetumia yuniti kadhaa,yuniti ya maji moja kila mamlaka ina gharama zake,mnapokwenda kusoma bili za Maji lazma mshirikishe mwananchi husika."-Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa Tanganyika katika uzinduzi wa Mradi wa Maji Majalila.
"Jukumu la Kumpatia maji Mwananchi ni jukumu letu sisi Wizara ya Maji kwa kutumia mamlaka zetu za maji lakini wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Mtanzania nae ana jukumu la kulipia bili za Maji pamoja na wajibu huo lakini bili hizo zisowe bambikizi,mtu ametumia Maji ya Sh 20,000 alafu anapewa bili ya Laki Moja na 80 kama vile ana kiwanda nyumbani kwake,haiwezekani."Aliongeza Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa Tanganyika katika mradi wa maji Majalila
Agizo hilo limekuja baada ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Ndg.Yasin Kibiriti alipopewa nafasi ya kuzungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Mh.Aweso alipotembelea Mradi wa Maji Majalila Mkoani hapa aliweza kutoa taarifa za uwepo wa mazoea ya wahusika wa Maji kumkadilia bili mwananchi pasipo kufika eneo lake huku akiziomba mamlaka husika kutengeneza utaratibu wa kusaini kwenye Daftari maalum la mwananchi endapo atafika eneo la tukio sanjali na kuweka kumbukumbu za usomaji wa Mita hizo.
Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanganyika Ndg.Yassin Kibiriti,kushoto ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso na kulia ni Mjumbe Kamati kuu CCM Taifa Ndg.Gilbert Sampa.
"Sisi tunaotumia Maji kuna wale wanaokuja kusoma Mita,Mara nyingi utapata ujumbe tuu ukisema umetumia shilingi kadhaa,kuna sehemu nyingine ukifikiria alikuja lini kusoma Mita hujui,kama ingewapendeza zaidi ili kuendelea kuboresha kungekuwa angalau na madaftari ili akija yule msoma Mita aripoti nimekuja tuliishia namba 20 na sasa ni 23 zimeongezeka 3 mwezi huu,anasaini pale unabaki na Kumbukumbu ili bili inapokuja mwananchi anajua na sisi tunajifunza namna ya matumizi ili tuendelee kuboresha vizuri miundombinu yetu ya Maji".Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Ndg.Yasin Kibiriti
Hata hivyo Mh Aweso amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka zote za Maji Nchini kuwa ikitokea Mwananchi atakaye katiwa Maji wakati amelipia bili za maji ndani ya masaa 24 anatakiwa arejeshewe maji hayo,na anapotaka kuunganishiwa maji pindi atakapokuwa amelipia maunganisho ya Maji,ndani ya siku 7anatakiwa Mwananchi yule awe ameshaunganishiwa Maji.
ReplyForward |
Comments
Post a Comment