Na Swaum Katambo,Site News
Mpanda,Katavi
Hali ya upatikanaji wa Mafuta ya Petroli Manispaa ya Mpanda sio shwari kutokana na kuadimika kwa Mafuta hayo huku wafanyabiashara waendesha vyombo vya moto ikiwemo bajaji na pikipiki wakilalamika kuomba utatuzi wa changamoto hiyo.
Mafuta ya Petroli Manispaa ya Mpanda yanapatikana katika kituo kimoja tuu cha Kampuni ya SERENIVA kilichopo Kata ya Majengo Manispaa hii huku Meneja wa Kituo hicho Thomas Magabe amesema kuwa shida ya mafuta imetokana na wauzaji kutoa Mafuta kidogo huku wakilazimika kutoa oda mapema kwenye visima vya matuta.
Baadhi ya wafanyabiashara vyombo vya Moto wakiwa kwenye kituo cha Mafuta SERENIVA
Nao wafanyabiashara wa vyombo vya moto hususan bajaji na pikipiki ambao ndio waathirika zaidi wamesema wanatumia muda mwingi kwenye foleni huku ikiwagharimu kibiashara na kupelekea hadi kupandisha bei ya kawaida ya usafiri iliyozoeleka.
Kwa upande wake Amani Mahela Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara na Mhasibu wa Kamati ya baraza la ushauri la Mkoa linalosimamia bidhaa zinazodhibitiwa na EWURA,amesema hali hiyo ya ufinyu wa mafuta imetokana na baadhi ya changamoto za usafiri kutokea njiani ikiwemo magari yanayosafirisha mafuta hayo kuharibika njiani huku akisema hadi ifikapo kesho August 4 tatizo hilo litakwisha
Ingia Youtube kujionea hali ilivyokuwa
https://youtu.be/2qjPzV4-mU8
https://youtu.be/2qjPzV4-mU8
#SiteNews
#TukutaneSite
#TukutaneKazini
Comments
Post a Comment