Skip to main content

RC KATAVI AWASWEKA MAHABUSU VIONGOZI GRAND TOBACCO NA KASOKOLA AMCOS,ACHARUKA HADI PESA ZILIPWE









Na Swaum Katambo,Site News

Mpanda,Katavi.

Kufuatia maagizo ya siku 10 aliyowahi kuyatoa katika kikao cha wadau wa uoteshaji wa Miti Katavi kuhusu Kampuni za PETROBENA na GRAND TOBACCO kuwalipa Fedha wakulima wa Tumbaku Mkuu wa Mkoa Juma Homera leo Aug 3 ameamuru kuwekwa mahabusu Viongozi wa Kampuni ya GRAND TOBACCO kwa kudaiwa zaidi ya Dola Laki 3 kwa zaidi ya Mwezi mzima.

"Nimeamuru Viongozi hawa wawekwe Mahabusu mpaka walipe hizo fedha,na hivi nnavyozungumza wameshapelekwa Mahabusu na wanaendelea kuhojiwa na vyombo vya sheria kuhakikisha kwamba fedha hizo hawatatoka ndani Mpaka walipe Fedha za wakulima ambazo zinatakiwa zilipwe baada ya kuchukua Tumbaku ya Wakulima".Alisema Mh Homera

Kwa upande Wa Kampuni ya PETROBENA yenyewe imelipa  Dola Laki moja na Elfu 40 huku wakidaiwa zaidi ya Dola Elfu 40 na Kampuni ya GRAND TOBACCO yenyewe haikulipa Kabisa huku Mh Juma Homera akisisitiza kutowaachia hadi pesa hizo zitakapoliwa.

Kwa upande mwingine Mh.Homera alisema kuwa kuna wananchi watano ambao bado hawajalipwa Fedha zao na Kasokola Amcos toka mwaka 2018 hadi hivi sasa wanaendelea kuzungushwa huku Amcos hiyo ikiwa na tuhuma za kuingiza majina hewa na kuuza Tumbaku kwa njia zisizo halali na kuacha Madeni kwenye Chama hicho cha Msingi hivyo madeni hayo kuhamishiwa kwa wakulima

"Tumeamua hao na bodi yao yote wawekwe Mahabusu mpaka walipwe hao wakulima watano ili tuweze kuhakikisha kwamba wananchi wanafurahia serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt.John Pombe Magufuli kwamba inatenda haki kwa wananchi" .Alisema

Kuhusu mustakabali wa wakulima Mh Homera amesema kuwa mpaka hivi sasa Kampuni ya PREMIUM  watanunua Tumbaku iliyobakia ambayo ilikuwa imesalia bado haijanunulika mpaka hivi sasa.

"Watanunua Tanganyika Amcos,Ilela Amcos na Mishamo Amcos baada ya mazungumzo na TTB (Bodi ya Tumbaku Tanzania) maana yake ni kwamba makampuni yaliyojiondoa kwenye kununua Tumbaku ya awamu ya pili yatanunuliwa na Kampuni nyingine". Aliongeza Mh.Homera

Comments

Popular posts from this blog

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja

Katavi Yakemea Vikali Ushoga,Mauaji "Wanaume Msiwazuie Wake Zenu Kufanya...