RC KATAVI APONGEZA WAKULIMA WALIOJITOKEZA KWENYE MAONYESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA,ASISITIZA NA UTALII
Na Mwandishi wetu,Site Tv
Nanenane-Mbeya
#NEWS Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera ameridhishwa na bidhaa za Wafanyabiashara kutoka Mkoani Katavi,baada ya kutembelea mabanda yao katika maonyesho ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayoendelea viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Homera akiwa ameambatana na Viongozi wengine akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu Abdalah Malela,Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda,Mh. Salehe Mhando wa Tanganyika na Jamilla Kimaro wa Mpanda baada ya kutembelea baadhi ya Mabanda amesema.
"Nimefarijika na namna maandalizi yalivyofanyika,kiukweli Mkoa wa Katavi wamejipanga vizuri,nimeona kwenye mabanda yao yanaridhisha,yanaendana na kauli mbiu ya Mheshimu Rais wetu Tanzania ya Viwanda,unaweza kuona wametengeneza Wine nzuri, wametengeneza unga mzuri, wametengeneza asali vizuri,na wana Viwanda vya asali kwa mfano ukienda kule Bulamata na maeneo mengine"-Alisema RC Homera, alipotembelea mabanda ya Nanenane.
"Lakini Manispaa nao wametengeneza bidhaa nzuri sana,kama vile neti n.k,hii inaonyesha kwamba Wananchi wamebadilika,na ndiyo maana siku zote nasisitiza lazima tuwe na siku ya Masoko ya ndani katika Mkoa wetu wa Katavi. Lazima tuwe na Siku 2 au Tatu za Masoko ya ndani,kwahiyo tutaainisha ni sehemu gani nzuri kwaajili ya kuuza bidhaa zetu katika Mkoa wa Katavi ili maisha yaweze kuendelea"-RC Homera,katika Viwanja vya Maonyesho ya Nanenane Jijini Mbeya.
Akiwa katika banda la Ofisi za Shirika la Hifadhi la Taifa Tanzania (TANAPA),Mh Homera ameshauri kuwepo na utaratibu wa upatikaji Nyama za Wanyama Pori ili kukata kiu ya Watanzania wanaopenda nyama hiyo.
"Mtu mpaka anazaliwa na anakufa hajawahi kula nyama ya Swala,sasa ni changamoto kubwa,Mimi nawashauri tu kwamba TAWA ndo mnazile WMA n.k,wekeni utaratibu ili nyama ziweze kupatikana,Watu wana hamu za nyama pori. Jambo lingine nyama ya Pori ni dawa,Mnyama pori anakula majani,majani yale yana virutubisho mbalimbali,akila na yeye anapata virutubisho,ndiyo maana Wazee wetu waliishi Miaka mingi kwa sababu walikula sana nyama za pori.-"RC Homera
Aidha,amewakaribisha Watanzania wote kwenda kutalii na kutembelea vivutio vilivyopo Mkoani Katavi ikiwemo Mto Mapacha,Twiga Mweupe,Viboko na Mamba.
-
"Mkoa wa Katavi kama mnavyofahamu tunavyo vivutio vikubwa vya utalii,ukitika Katavi ndiyo unakutana na Twiga Mweupe,ukifika Katavi unakutana na Viboko zaidi ya Elfu Kumi,na ndiyo hifadhi yenye Viboko wengi Tanzania"RC Homera,Katika Maonyesho ya NaneNane Jijini Mbeya
"Lakini pia utakutana na Mamba,Mamba watulivu lakini wakali,ukifika Katavi utakutana na Maji ya Mto Mapacha,ukipata yale Maji unauwezo wa kuzaa Mapacha,zaidi ya Kaya 30 mpaka sasahivi tunavyozungumza,zilikuwa Kaya 28 na zinazidi kuongezeka wanazaa Mapacha,kwahiyo Ndugu Waaandishi wa Habari Mimi nawakaribisha sana"-Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera
"Kama unahitaji Watoto mpigo mpigo,basi unaweza ukaja ukapata Maji ya Mto Mapacha ukanywa Wewe na Mpenzi wako mkazaa Mapacha,na wale Watoto Mapacha sio misukule,ni Watoto halisi kabisa kwasababu wapo na wanaakili timamu kabisa,na yale Maji ni mazuri kabisa."-Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera.
#SiteNews
#TukutaneSite
#TukutaneKazini
Comments
Post a Comment