MWALIMU WA SHULE YA MSINGI MKOANI MBEYA ADAKWA KWA TUHUMA ZA WIZI KWA NJIA YA MTANDAONI KIASI CHA MILIONI 34.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya,Ulrich Matei akionyesha Pesa zilizokamatwa. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA WIZI KWA NJIA YA MTANDAO. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia JOSEPH SHILA [29] Mwalimu Shule ya Msingi Mwakareli na Mkazi wa Mwakareli kwa tuhuma za wizi wa fedha Tshs.Milioni 34,000,000/= mali ya mwalimu mstaafu GIDEON NGOLAKO MWALUJOBO [60] Mkazi wa Mwakareli. Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 30.06.2020 majira ya saa 19:00 Usiku huko Kijiji na Kata ya Mwakareli, Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya baada ya kupata taarifa toka kwa msiri. Mtuhumiwa alifanikiwa kuiba pesa hizo mali ya mwalimu mstaafu GIDEON NGOLAKO MWALUJOBO [60] Mkazi wa Mwakareli kupitia akaunti 6140201871 kwa kutumia “NMB Mobile” katika Tawi la NMB Mbalizi ...