Mtoto mmoja aliyefahamika kwa majina ya Trifon Filbert Kanoni (5) amefariki Dunia kwa kuzama kwenye bwawa la kufyatulia tofali lililopo Eneo la mnazi mmoja E,kata ya uwanja wa ndege tarafa ya kashauriri manispaa ya Mpanda mkoani katavi.
Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya mashuhuda wa tukio Hilo wamesema tukio limetokea Juni 24,2020 majira ya saa 7 mchana wakati alipokwenda kumtembelea baba yake mdogo anaejihusisha na shughuli za uchomaji Matofali.
Dada wa Marehemu huyo,Anasitazia Martin amesema,Mdogo wake huyo hakuwa anasoma huku Baba wa Marehemu, Filbert Kanoni akieleza kuwa alipata taarifa majira ya saa Sita mchana na kufika eneo la tukio lakini alikukuta Mtoto wake ameshafariki Dunia tayari.
Nae Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo Juma Gogomoka amewaasa wazazi kutowaruhusu watoto wao kujishughulisha na shughuli za Matofali huku akiwaasa wachomaji kuacha tabia za kuwapa ajira watoto ili kuwalipa pesa ndogo ambayo ni sh 5 kwa Kila tofali.
Kwa upande wake Afisa Oparesheni wa zima Moto Paul Masungwa ametoa ushauri kwa wananchi kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa kwa wakati kwa kupiga simu ya bure 114 na kuwaomba viongozi wa serikali ya Mtaa kuwasimamia wafyatuaji matofali wafukue madimbwi ambayo ni hatarishi.
Aidha,amesema Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Katavi linaendelea kutoa elimu kwa Jamii ili kujua namna ya kujiepusha na majanga kama hayo ikiwemo utoaji taarifa mapema.
Taarifa zaidi,tembelea YouTube channel yetu @sitetvtz
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_jUnmkpfSYyd0TUyd9G1roecsrGVP8Fhk-8Pb6XUgqDP_pTiwOrsn9r0VOFE1wBDzT5H_KdRlq7QuYi_1GMAIam2Izk8fl9Lv3Ri8G2xr2Tk_DBZWMfXcQDQiwC051ycQO0rfVY-uJrI/s320/IMG-20200625-WA0006.jpg)
Anasitazia Martin,Dada wa Marehemu
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3pULQajPfgvV4mQgg4a6Gb7etzJ5-DG2Y7goMy3h37-pkd1cCK4HAC_orYS22Xzn0cGQfWRcOKS-90FdZdg9CYhrjpzB-MNtgFBXFD7_IuUMAQtHehzkhyphenhyphenzs92aSxPJm93gqoBut3Nwk/s320/IMG-20200625-WA0008.jpg)
Filbert Kanoni,Baba wa Marehemu
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhfbli01OXXezNY-d1uTIJNHUGL4pvgmepZUPioWrcCVtP8FCKaSFh33wMlQD1KiRSL7IMUlPchjr-ZBb-De8N7NUFV5wO1gv5hAfoen4fWz8OPTFnWBzOE1NhO7nLcPtCMjq26cFhX5n4/s320/IMG-20200625-WA0011.jpg)
Afisa Oparesheni wa zima Moto,Paul Masungwa
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjHwYzfLZFUh_Gqdn_5jdaI75ksOONbP3hwD1e1E29VliGDWENiCxYVaexgMl8B5_6-AttZ4VaCRlDhTaisjXS7_Np1eBOmEs8aV0BhK3EF1rzKU58iCJ2UZcw24kwJ3w4J7LZuCJBHnTM/s320/IMG-20200625-WA0007.jpg)
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa,Juma Gogomoka
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhUAVla1CHlsza2MlfmauT7NED0Tm_q8B5kQRN7m-0PAD5qbMuuQ3ZT2V78hKuW4Ojco8udr3mE927EQg_H5-7ZZBCotCBMBkql1Jtb38_oekzOXXdY0zTBToiUt2DojFNd0-3k50kj-oQ/s320/IMG-20200625-WA0009.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGlcXn-qmC9p_VlbMfh88TKfMtPpo5H7Kp644Jg5S9MiT-p3cMjCMtfrDoN3hWBReSFZ3jxDJjemgIeVE3jH-18UZMA2fxE_5gMRAaQYiS6MHfkIu4WAkTQ2SKpA0Vqos2iNTXHl1hGWU/s320/IMG-20200625-WA0010.jpg)
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgJpRXfdOgSJpL2xI8dqnxapflTXKk4AM71Wbe4QigeMOBTNIJLRAGvLmclsM75AEc75moDCxkzIj4i_aKAJu-5QvOm1iteJ4w9scpH-x68FJw2m9Y_7xvr8LmM8IQ9lC1kMNyH-sLAB0s/s320/IMG-20200625-WA0012.jpg)
Bwawa lililopelekea kifo cha Mtoto huyo
Comments
Post a Comment