Mkoa wa Katavi umetenga zaidi ya Ekari 200 eneo la Kabungu Wilayani Tanganyika kwaajili ya kuanzisha Maonyesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane) za mwaka 2021 ambapo kabla ya mpango huo Wakulima kutoka Mikoa ya Nyanda za juu Kusini iliwalazimu kwenda Mkoani Mbeya.
Akizungumza na Site Tv ilipokwenda kuangalia maendeleo katika eneo hilo Msanifu Majengo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Ndg. Iblahim Bashiru amesema hadi sasa maandalizi yako hatua ya kwanza ya kulisafisha eneo pamoja na kuchonga Barabara.
"Shughuli zinazofanyika hapa,kwanza tuna eneo la Ekari 221 ambapo katika eneo hili tutakuwa na majengo ya Halmashauri,tutakuwa na maeneo kwaajili ya zana za Kilimo na Taasisi mbalimbali"-Ibrahim Bashiru,Msanifu Majengo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
"....hapa ni uchongaji wa Barabara za kuingia ndani ya site kwa maana ya access road pamoja na main Road,tunachokifanya kwa sasa ni awamu ya kwanza ya usafishaji eneo na kuonyesha mipaka ya Barabara pamoja na maeneo husika"
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjAK5CXrYY5IF2Al1YKTHKsADHhBFFewvMPaQeEwteElbI1CL5cl8lGj9hs9igYBg1Ehxp7Uj57OO7UqUwHxxamTez-ujBM8_Q68QrDZHNxpM8yjwkJdjtU-vhI4uMFnmVt0Yb5EHQObOQ/s640/IMG-20200626-WA0153.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhuJtT7_Su1-ujAVY2WywfkupYcD8W1yUxgbRRM1iAdog-JbMyqMooQJTDQ2yHMuKMRMp4cqlvtdIVg9FmCrbg0bOsTbj74Kp3qCP6kRGDMM2eqrBMmZ3pLIV7uUGwyursVsn3h9iBeVZk/s640/IMG-20200626-WA0152.jpg)
Trekta likiendelea kusafisha eneo lililotengwa.
Kwa upande wake Kaimu Nkurugenzi Wilaya ya Tanganyika Ndg. Samson Medda alisema lengo la kuanzisha Maonyesho hayo ni kusogeza Elimu zaidi kwa Wakulima juu ya mbinu mbalimbali za Kilimo.
Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Salehe Mbwana Mhando naye pia alisema kuanzishwa kwa viwanja vya Nanenane Mkoani Katavi ni msukumo wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Juma Zuberi Homera kwa kutambua kuwa Katavi ni Mkoa wa Kilimo.
"Tupo kwenye eneo hili la Kabungu ambapo ndipo eneo lilipotengwa kwaajili ya uanzishwaji wa maonyesho ya Nanenane Kikanda,ambapo maonyesho yatakuwa katika Mkoa wetu wa Katavi na kama mnavyoona tuko site,maandalizi yameanza,na kwa maelekezo ya Mh Mkuu wetu wa Mkoa Comred Juma Zuberi Homera ambaye amekuja na msukumo huo,kuhakikisha kuwa Mkoa wetu ambao ni wa Kilimo na ni mkoa wa nne kwa uzalishaji,kwahiyo tunataka tuitafsili hii dhana ya uzalishaji katika sekta ya Kilimo kwa kusogeza hii huduma ya maonyesho ya Nanenane"-Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika,Salehe Mhando.
Mhando aliongeza kuwa,lengo la mradi huo ni kuongeza uzalishaji wenye tija ambao utakwenda sambamba na kuanzisha kiwanda ili kujenga mnyororo wa thamani.
"Hakuna kulala usiku na mchana mpaka hii dhamira iweze kutimia....ujio wa huu mradi ni kutaka kuhakikisha kwamba tunaongeza uzalishaji,lakini uzalishaji wenye tija ambao utakwenda sambamba na uanzishwaji wa Viwanda ili kujenga mnyororo wa thamani kwa mazao ya Wakulima,mazao ya Mifugo na Uvuvi ili kuhakikisha pia kwamba tunatumia vizuri fursa ya kupakana na Nchi jirani ya Congo"-DC Mhando
Comments
Post a Comment