![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella akipokea Matanki matano kutoka wa wadau wa mapambano ya COVID 19 jijini humo |
Na Mwandishi Wetu
Tanga
MKUU wa Mkoa
wa Tanga Martin Shigella amepokea vifaa vya kujikinga na ugongwa wa COVID 19
ikiwa sambamba na kuwataka wafanyabiashara wengine kuguswa na kuchangia vifaa
vya usafi ili kuhakikisha wanadhibiti na kuchukua hatadhati za kujikinga na
ugonjwa huo.
Kauli hiyo ameitoa wakati
akipokea msaada wa mataki matano ya ujazwa wa lita mia tano kila moja kutoka
kampuni ya vifaa vya ujenzi ya Hussain Plastic Industry ya jijini hapa.
Shigella amasema bado
kunauhitaji mkubwa wa vifaa kwa ajili ya kusabazwa kwenye maeneo mengine ya mkoani Tanga ili
wananchi waweze kujikinga na COVID 19 kupitia kunawa mikono kwa maji safi
yanyotiririka .
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo
Hussein Yusuph amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kuuga juhudi juhudiza
serikali katika mapambano katika kukabiliana na ugonjwa huo
Hata hivyo ametoa wito kwa
wananchi wengine wenye uwezo wa kuguswa na tatizo hilo wapatwe na msukumo wa
kutoa msaada ili kuenndelea kujikinga virusi vya Corona visivyo na mashika.
“Sisi kama sehemu ya jamii
ya Tanga tumeona tuugane na serikali katika kuhakikisha tunashirikiana kuchukua
tahadhari dhidi ya COVID 19”alisisitiza Yusuph.
Aidha baadhi ya wakazi wa
Jiji hilo Athony Charles na Aisha Ramadhani wameipongeza serikali ya Mkoa kwa
kuendelea na juhudi za kuwaelimisha wananchi kujikinga na ugojwa huo
hatari.
Comments
Post a Comment