Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ChristinaMndeme akikagua mradi wa maji wa Mkongogulioni Wilayani ya Namtumbo.
SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imetoa zaidi ya Tsh. Bilioni Mbili ili kutekeleza mradi wa Maji wa Mkongogulioni na Nakahimba Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Namtumbo David Mkondya akitoa taarifa ya mradi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme,amesema mradi huo ulisainiwa Juni 12 mwaka 2013 na utekelezaji wake ulianza mwaka 2017 na ulitarajiwa kukamilika Februari 2020 chini ya Mkandarasi Kipera Contractors.
Mkondya alisema mradi huo unatarajia kuhudumia watu zaidi ya 8000 katika vijiji vya Mkongogulioni na Nahimba na kwamba kazi ambazo zimepangwa kufanyika kwenye mradi huo ni ujenzi wa tanki la lita 25,000 katika kijiji cha Nahimba na ukarabati wa matanki mawili yenye ujazo wa lita 150,000 katika kijiji cha Mkongo.
Hata hivyo alizitaja kazi ambazo zimefanyika kulingana na mkataba kuwa ni uchimbaji wa mtaro katika kijiji cha Nakahimba ambao umefikia zaidi ya asilimia 83,ujenzi na ukarabati wa matanki ya kuhifadhia maji,ujenzi wa chanzo,ulazaji wa mabomba na ujenzi wa vituo 46 vya kuchotea maji.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema ameridhishwa na mradi huo na kusisitiza kuwa serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 30 kutekeleza miradi ya maji katika Mkoa wa Ruvuma.
Ali
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Juni 28,2020
Comments
Post a Comment