Skip to main content

MKOA WA KATAVI UMEJIPANGA KULETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI KWA KUONGEZA VIWANDA,KUKUZA SEKTA YA MADINI NA KILIMO.




Na Swaum Katambo

Mpanda-Katavi

Kuelekea mwishoni mwa Mwaka wa fedha,Mkoa wa Katavi umejiandaa kuleta mapinduzi makubwa ya Kiuchumi ikiwemo kuongeza Viwanda,kuongeza Vyuo,kukuza sekta ya Madini,Kilimo na Umeme Vijijini.

Akitoa mwelekeo wa Mkoa,Mkuu wa Mkoa Mh. Juma Zuberi Homera katika kikao na Waandishi wa Habari kilichofanyika Ofisini kwake Juni 24,2020 amezungumzia mwenendo wa Soko la Madini na mikakati ya kuongeza kasi ya ununuzi na uuzaji wa Madini.

Kuhusu Madini Mh Homera alisema,toka Soko la Madini lianze Mei,2019 hadi Juni 2020 Mkoa umefikisha Kilogra 254 za Madini na Gram 734 zenye thamani zaidi ya Tsh. Bilioni 24 ambapo kupitia soko la Madini Mkoa umeshakusanya kiasi cha Tsh. Bilioni 1.7 huku tozo za huduma kutoka katika Sekta ya Madini ikichangia zaidi ya Milioni 66.

Alisema matarajio ni kuhakikisha ongezeko la ununuzi na uuzaji wa madini,na Serikali imeshapata eneo la uchimbaji Madini la zaidi ya Hekta 1901 kutoka kampuni ya Kijani Investment ambapo Hekta 701 zimeshatumika na wachimbaji wadogo,huku akisisitiza Wananchi kuuza Madini katika Soko la Madini ikiwemo kuacha tabia ya kuyatorosha.

Katika kukuza zao la Pamba,Serikali ya Mkoa kupitia Kampuni ya NGS inajenga Kiwanda cha Kuchakata Pamba eneo la Kabungu Wilayani Tanganyika chenye uwezo wa kuchakata Tani Elfu 50 kwa Mwaka ambacho kinatarajiwa kuzinduliwa Mwezi Julai Mwaka huu hivyo Pamba haitasafirishwa ghafi kama ilivyokuwa awali na ameongeza kuwa wanunuzi wameshapatikana na kila Mkulima atalipwa fedha zake kwenye Akaunti au kwenye simu kwa kufuata bei elekezi.



Aliongeza kuwa,Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa 2 ambayo imepewa kazi ya kuandaa Mbegu za Pamba kwa Nchi nzima na amesema Mkoa unatarajia kuzalisha Tani Elfu 14 hadi Tani Elfu 15 kutoka katika Halmashauri za MKoa,huku akiishukuru Bodi ya Pamba Nchini kwa kuiondolea kizuizi Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kulima Pamba.

Aidha,alizungumzia soko la Tumbaku ambapo Mkoa unatarajia Kuzalisha zaidi ya Kilogram Milioni 6 kwa msimu wa kilimo 2019/20 na zaidi ya Kilogram Milioni 1 na Laki Nne zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 4 zimenunuliwa na Makampuni ya PREMIUM na Grand Tobacco,huku akisema soko la Ufuta  limeshuka kutokana na Soko la Dunia.

Mh. Homera alizungumzia pia hali ya Mapato kwa kila Halmashauri na mwenendo wa ugawaji wa Vitambulisho vya Ujasiriamali ambapo Mkoa ulipata Vitambulisho Elfu 30,Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeongoza kwa kugawa Vitambulisho Elfu 1,439 vyenye thamani ya Tsh. Milioni 28,780,000 sawa na Asilimia 19.19 kati ya Vitambulisho 7,500 ilivyokabidhiwa,Manispaa ya Mpanda imeshika nafasi ya Pili na imegawa Vitambulisho 1,398 sawa na Asilimia 11.65 vyenye thamani ya Tsh. Milioni 27,987,450 kati ya Vitambulisho Elfu 12 na Halmashauri ya Mlele imegawa Vitambulisho 913 sawa na Asilimia 8.70 na wameshakusanya kiasi cha Tsh. Milioni 18,260,000/= kati ya Vitambulisho 1,500.

"Mpaka hivi sasa maana yake Mkoa umeshakusanya Bilioni 8 na Milioni 127,Laki Saba Sitini na Sita Elfu,Mia Tisa Ishirini na Sita Nukta 69,mpaka tunafikia tarehe ya leo tuko zaidi ya 90%  hayo ni mafanikio makubwa kutokana na makusanyo makubwa ambayo tunayakusanya kwenye mazao,kwa kuuza mazao kwa mtindo wa vituo,lakini pia kwa mfumo wa Stakabadhi ya Mazao ghalani lakini pia kwa kubana mianya yote ya upotevu wa mapato katika Mkoa wetu wa Katavi"-RC Homera.

Kuhusu Umeme wa REA,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera alitoa siku 20 kwa mkandarasi wa Kampuni ya CHINA RAILWAY CONSTRUCTION ELECTRIFICATION BUREAU GROUP ( CRCEBG) ahakikishe anawasha Umeme katika Vijiji vya Karema,Ikola na Kapalamsenga vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.

"Kunachangamoto kubwa sana,ukiangalia Umeme wa REA tunajenga Bandari ya Karema kwa zaidi ya Bilioni 47 na Point,lakini Umeme bado haujafika,tunamuagiza Sisi mkandarasi,Sisi tunampa siku 20 awe ameshawasha Umeme Karema,awe amewasha Umeme Ikola,awe amewasha washa Umeme Kapalamsenga,maeneo hayo ni Strategic area kwa Nchi yetu"-RC Homera
 
Hata hivyo,alieleza kuwa katika Sekta ya Afya,huduma zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa Mkoani humo kwa kuwasogezea Wananchi huduma karibu ambapo alisema Hospitali zote za Wilaya zimeanza kufanyakazi na vituo vyote vya Afya vinatoa huduma.

"Mpaka tarehe ya leo Hospitali zote za Wilaya zilizojengwa na Dkt. John Pombe Magufuli chini ya Ilani ya CCM ya mwaka 2015/20 zimeanza kufanya kazi,na vituo vya Afya vyote vilivyojengwa chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ndani ya Mkoa wa Katavi tayari vinatoa huduma za Afya,na katika vituo hivyo 8,vituo takribani 7 vinatoa huduma ya upasuaji"-RC Homera

Amewakaribisha Wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali kuja kuwekeza katika Mkoa wa Katavi huku akitoa rai kwa Wazazi kuendelea kuwalinda Watoto dhidi ya Virusi vya Corona wakati wanafungua Shule,na amezionya Shule zote zitakazowazuia Watoto kuanza masomo kwa sababu zozote bila taarifa na ameeleza mikakati ya Mkoa kuongeza Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati.

"Nawakaribisha wawekezaji waje kwasababu kwenye sekta ya Kilimo,sekta ya Afya,sekta ya Utalii sababu tunayo hifadhi kubwa ya Katavi ambayo inaendelea kuimarika zaidi,lakini tunayo Hifadhi mpya ya Ugala,Mto Ugala ambayo ipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na Nsimbo kwa kiasi flani"-Juma Homera,Mkuu wa Mkoa Katavi.

"Mwaka huu,Mwaka 2020 tunafungua Vyuo 2 Vikuu,Chuo cha Madaktari Msaginya hivi karibuni Wizara ya Afya itapokea Chuo cha Afya kilichopo Mpanda na tayari wameshatangaza maombi ya Wanafunzi kwa ajili ya kukifungua Mwaka huu, huu ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/20 kuendelea kufungua Vyuo Vikuu na vya Kati"-RC Homera

"Lakini pia mwezi wa 11 huo huo,tunafungua Chuo Cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda Kibaoni, zaidi ya Wanafunzi Mia Nne wataingia pale kwa Chuo cha Afya wataanza na Wanafunzi karibu 150 lakini Chuo cha SUA Kampasi ya Mizengo Pinda zaidi ya Wafunzi 400 wataanza katika chuo kile na tayari ukarabati umesha kamilika na Wanafunzi registration itanza maana yake ni kwamba tayari Chuo kinaanza ndani ya Mkoa wetu wa Katavi tutakuwa na Vyuo vya Kati 2 na Vyuo vidovidogo vya kutosha"-RC Homera

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...