Skip to main content

Posts

MGANGA MKUU WA MKOA WA KATAVI ATAKIWA KUJIELEZA KWA KUKIUKA AGIZO LA RC HOMERA DHIDI YA CORONA.

Ni baada ya wahamiaji haramu watano waliokamatwa na maafisa wa uhamiaji kushindwa kufanyiwa vipimo. Na Mwandishi Wetu,       Katavi. MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Omary Sukari anapaswa  kujieleze kutokana na kukiuka maagizo aliyopewa March 28 mwaka huu kwenye kikao cha dharura PHC cha maelekezo ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona., Kikao hicho ambacho kililenga pia kusambaza muongozo wa karatini kwa wageni wote wanaoingia mkoani humo kupitia njia mbali mbali za usafiri kama vile wa mabasi na meli ambapo yalitolewa maadhimio ya kuhakikisha kila eneo la mpaka wa Mkoa linakuwa na kituo  maalumu cha kizuizi kwa ajili ya ukaguzi wa kitabibu na karatini pamoja na wataalamu wa afya ili kabla ya mtu hajaingia mjini apimwe kwanza. Akitoa kauli hiyo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Comrade Juma Homera baada ya kufanya  ukaguzi wa kushitukiza ili kuona utekelezaji wa maagizo yake katika kituo cha kizuizi ...

MWENYEKITI WA KIJIJI KWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUOMBA RUSHWA YA LAKI MBILI.

    Na Mwandishi wetu           Katavi . TAASISI ya kuzuia na kupambana  na Rushwa(TAKUKURU)  Mkoa wa  Mkoa wa Katavi  inatarajia kuwafikisha  Mahakamani watuhumiwa watatu waliowakamatwa  wakitenda makosa ya kuomba na kupokea Rushwa  kinyume na  kifungu  cha 15(1)  (a) na (b) cha sheria  ya kupambana na Rushwa  namba   11 ya mwaka 2007 akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Vikonge Wilaya ya Tanganyika  Joseph  Sungura (53) aliyekamatwa kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya Tshs 200,000. Mkuu wa Takukuru  Mkoa wa Katavi  Christopher  Nakua  aliwaambia wandishi wa Habari kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo tofauti ya Wilaya  za Mpanda na Tanganyika .  Katika tukio la kwanza Takukuru  ilimkamata  Mwenyekiti wa Kijiji cha Vikonge  ambae anadaiwa  alimwita kwenye ofisi yake  mlalamikaji wa tukio...

MAMANTILIE WACHANGIA FEDHA MAPAMBANO YA CORONA ,WAZIRI MKUU AKOLEZA VITA YA COVID-19

Na Mwandishi wetu       Dar es salaam. WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba watu wote nchini kuendelea kukabiliana na ugonjwa wa corona ili kuzuia kusambaa zaidi. Hayo ameyasema waziri mkuu huyo baada ya kukabidhiwa vifaa kinga,fedha na dawa kutoka taasisi,Mampuni na Umoja wa Mamantilie . Kassim Majaliwa amesema kuwa watanzania wanapaswa kuzingatia kuchukua tahadhari kama vile kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi na salama yanayotiririka pamoja na kuepuka misongamano ili kudhibiti janga lililoikumba dunia. "Wakati tunaendelea kukabiliana na janga hili la corona tunapaswa kujua kwamba ugonjwa huu utaleta athari za kiuchumi " amesema Majaliwa. Hivyo pia amewashukuru watanzania waliojitokeza kuchangia fedha,dawa na vifaa kinga kwa kuwa msaada huo utakuwa na tija kwa watu wote waliokumbwa na COVID-19 pamoja na kusaidia watu wote kujikinga ili kuzuia kusambaa kwa homa kali ya mapafu. Amesema Waziri Mkuu "Vitu vyote hivi tuliv...

RC HOMERA ATAKA TAHADHARI ZAIDI DHIDI YA CORONA

Na Mwandishi wetu.       Katavi KATIKA juhudi zinazofanywa na serikali ya Mkoa wa Katavi za kuendelea kukabiliana na Virus vya Corona (COVID-19) imeadaa mpango wa dharura wa kukabiliana na ugonjwa huo ambao unahitaji jumla ya fedha Tsh 856 milioni. Akizungumza katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani humo kwenye  kikao cha dharura PHC cha maelekezo ya namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona na kusambaza muongozo wa kataratini kwa wageni,Mkuu wa Mkoa huo Comrade Juma Homera amesema janga la ugonjwa huo linapaswa kushughurukiwa ipasavyo. Ameweka wazi kuwa suala la mpango wa dharura ni muhimu katika kuendesha mapambano dhidi ya virus vya Corona huku akisema kuwa mpango huo tayari umeshatumwa Wizara ya Afya pamoja na OR-TAMISEMI. Amebainisha kuwa kila halmashauri za mkoa wa Katavi imeelekezwa kutenga kituo kimoja kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa sambamba na hilo kila kituo cha kutolea huduma kimeelekezwa kutenga chumba maalum ya kuwaweka wahisi...

JPM AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI OFISI NDOGO YA CCM MTAA WA LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM/AKUTANA NA MASHINJI

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Ofisi Ndogo ya chama hicho tawala mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Februari 28, 2020 Viongozi waandamizi watano kutoka vyama vya upinzani wakitambulishwa na kupokelewa rasmi kuwa wana CCM mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wajumbe wa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Ofisi Ndogo ya chama hicho tawala mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Februari 28, 2020. Kutoka kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji, aliyekuwa Meya wa jiji la Arusha kupitia CHADEMA Bw. Kalisti Lazaro,  aliyekuwa Meya wa Jiji la Mbeya kupitia tiketi ya CHADEMA Mchungaji David Mwashilindi, aliyekuwa Mbunge wa Tandahimba kupitia CUF, Bw. Katani Ahmed Katani na aliyekuwa Naibu Meya wa Jiji la Mbeya kupitia tiketi ya CHADEMA Bw. Fan...

TWENZETU KATAVI

Twenzetu Kutalii nyote mnakaribishwa kinyumbani zaidi

POLISI KATAVI WAMEWAKAMATA WAHALIFU NA SILAHA ZA KUTISHA

Mkoa wa Katavi wakamata wahalifu wa ujangili 17 wa mbao na Nyamapori Raia wa Burundi na silaha 50 aina ya SGM 13,G3 idadi 3,Rifle 1 na Gobole 33 na kubaini mafundi wanao tengeneza Silaha aina ya Gobole eneo la Katumba na mishamo katika makazi ya Raia wapya kutoka Burundi waliopewa uraia na mbali na silaha lisasi 28 zimekamatwa, kamba za kutegea wanyama zaidi ya 20, Akizungumza mkuu wa mkoa wa Katavi Comrade Juma Zuberi Homera kwamba, oparesheni hiyo iliyodumu Siku 21 ilijumuisha vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na taskforce ya mkoa huo. Author : Mkutubi26 Publisher : Pizo