Na Mwandishi wetu
Katavi .
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Mkoa wa
Katavi inatarajia kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa watatu waliowakamatwa wakitenda makosa ya kuomba na kupokea Rushwa kinyume
na kifungu cha 15(1) (a) na (b) cha sheria ya
kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 akiwemo Mwenyekiti
wa Kijiji cha Vikonge Wilaya ya Tanganyika Joseph Sungura (53)
aliyekamatwa kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya Tshs 200,000.
Katika
tukio la kwanza Takukuru ilimkamata Mwenyekiti wa Kijiji cha
Vikonge ambae anadaiwa alimwita kwenye ofisi yake mlalamikaji
wa tukio hili ambae alikuwa akifanya kazi kijijini hapo ya kununua
mazao kwa niaba ya tajiri yake anaeishi Dar es salaam ambae wakati
wa ununuzi wa mazao hayo alikura hasara na kushindwa kurudi kwa tajiri
wake
Nakua
alieleza kuwa ndipo Mtuhumiwa Joseph Sungura alipomfuata
mlalamikaji na kumweleza kuwa anatafutwa na tajiri yake
hivyo ili yeye Mwenyekiti aendelee kumlinda anatakiwa
ampatie kiasi cha Tshs 200,000 .
Kwa
kuonyesha msisitizo wa mahitaji ya fedha hizo mtuhumiwa
alimnyang'anya mlalamikaji baiskeli aliyokwenda nayo kwenye ofisi
ya Kijiji hicho ikiwa na pampu ya kunyunyizia dawa za
wadudu .
Nakua alieleza kuwa Takukuru walipata taarifa za mwenyekiti huyo
kuomba Rushwa na kuwa amenyang-anya mlalamikaji baiskeli
yake waliweza kufika hadi nyumbani kwa mtuhumiwa na waliweza
kuvikuta vitu hivyo na alipo ulizwa hakuwa na maelezo yoyote .
Mtuhumiwa
anatarajiwa kufikishwa leo Mahakamani kwa tuhuma za kushawishi na
kuomba rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) (a) cha
sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka
2007.
Katika
tukio jingine Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi amesema wamewakamata watu wawili Justina Mgamba Mkazi
wa Kijiji cha Kanoge Wilaya ya Mpanda na Mohamed Kajenje
Mkazi wa Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika watuhumiwa
hao ni wajumbe wa jumuia ya Bonde la Mto
Mpanda waliomba na kupokea Rushwa ya Tshs 50,000.
Alisema
watuhumiwa hao mnamo machi 18 mwaka huu wakiwa katika
operesheni ya kuwaondoa na kuwaadhibu watu
waliolima na kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya eneo la mita
60 kutoka kwenye bonde la mto mpanda walimkuta mlalamikaji akiwa amelima
ndani ya mita 60 kutoka kwenye mto .
Ambapo
kulingana na sheria ya usimamizi wa rasilimali maji
namba 11 ya mwaka 2009 alitakiwa kulipa faini kati ya Tshs 500,000
na 1,000,000 lakini watuhumiwa hao waliomba na kupokea rushwa ya
Tshs 50,000 ili wasimlipishe faini kubwa ndipo Takukuru
walipopata taarifa na waliandaa mtego na kufanikiwa kuwakamata .
Nakua
alisema watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa kosa
la kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha
15(1) (a) na (b)
cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya
mwaka 2007.
Comments
Post a Comment