Na Mwandishi wetu
Dar es salaam.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba watu wote nchini kuendelea kukabiliana na ugonjwa wa corona ili kuzuia kusambaa zaidi.
Hayo ameyasema waziri mkuu huyo baada ya kukabidhiwa vifaa kinga,fedha na dawa kutoka taasisi,Mampuni na Umoja wa Mamantilie .
Kassim Majaliwa amesema kuwa watanzania wanapaswa kuzingatia kuchukua tahadhari kama vile kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi na salama yanayotiririka pamoja na kuepuka misongamano ili kudhibiti janga lililoikumba dunia.
"Wakati tunaendelea kukabiliana na janga hili la corona tunapaswa kujua kwamba ugonjwa huu utaleta athari za kiuchumi " amesema Majaliwa.
![]() |
Amesema Waziri Mkuu "Vitu vyote hivi tulivyo vipokea vinagharama kubwa,tumeona watanzania wenye moyo wamekuja hapa kuugana na serikali kukabilia na ugonjwa huu,Hivyo hatuwezi kuacha hivi bila kutoa shukrani kwa wenzetu walio toa msaada huu".
Amefafanua kuwa watanzania wanaopenda kuchangia jitihada za kukabiliana na ugonjwa huu wachangie fedha Benki Kuu kupitia Account NATIONAL RELIF FUND ELECTRONIC,Namba 9921159801 na kwamba wanaweza kuchangia kupitia Ofsi ya Waziri Mkuu na Ofsi ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto.
Baadhi ya Kampuni zilizochangia serikali katika kukabiliana na corona ni NMB mil 100,CRDB mil 150,Benk ya UBA mil 230,Umoja wa Mamantilie Mil 2 ,ASHTON MEDIA mil 104 na kampuni mbalimbali zimechangia fedha nna vifaa.
Wakati huo huo waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsi wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa kwa kipindi cha masaa 24 tangu March 27 Mwaka huu jumla ya sampuli 26 zimewasilishwa maabala ya Taifa ya Afya ya jamii na zote zimethibitishwa hazina maambuki(hasi) Hivyo watu walio thibitika chanya kuwa na ugojwa huo bado ni 13.
Comments
Post a Comment